Mkazi
wa kijiji cha Nakachindu kata ya Mkundi Halmashauri ya wilaya ya
Masasi, Asumini Bakiri (39) amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la
mauaji linalomkabili la kumuua mumewe, Simoni Simoni (45).
Alifikishwa
mahakamani jana na kusomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka, Iddi
Shabani mbele ya Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Masasi, Halfani Ulaya.
Alidai
kuwa mshtakiwa huyo, alitenda kosa hilo Januari Mosi mwaka huu huko
katika kijiji cha Nakachindu wilayani Masasi saa 1:00. Anadaiwa kumuua
kwa kile kinachodaiwa ni sumu baada ya kutokea ugomvi kati yao.
Iddi
alidai kuwa siku ya tukio, mume alinunua mapupu yanayoliwa pamoja na
nyama ya mbuzi nusu kilo kwa ajili ya sherehe ya Mwaka Mpya, lakini
katika hali ya kushangaza usiku ulipofika alihitaji chakula, lakini
mkewe alidai kuwa hakuna unga na kwamba angeenda jirani kuomba.
Akiwa
ametoka nyumbani kwenda jirani kuomba unga huo, mume alianza kula nyama
na baada ya kumaliza alianza kutokwa na povu jeupe kinywani mithili ya
mtu aiyepewa sumu huku hizo nyama zikiwa zimekwama shingoni mwake.
Mkewe
alipofika alimkuta mumewe akiwa ameshapoteza fahamu na alifariki dunia
akiwa kwenye pikipiki, wakati akipelekwa hospitali kwa ajili ya
matibabu. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Simoni aliwekewa sumu kwenye
nyama hiyo.
Mshitakiwa alirudishwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Januari 19 mwaka huu itakapotajwa tena.

Post a Comment