OYA KACHAA USIKATE TAMAA KAZA JOMBAA!

Wanangu Saa Godi mkubwa masela. Kwa mkono wake tumevuka kitu cha brandi niu yia 2015! Dheni cha kufanya ni kumpigia goti. Ama nini? Basi barida! Kipande hiyo ishu zikoje makachaa? Maana sipati picha hilo bata linavyoliwa kijanja. Yap! Kijanja kozi ukitaka ulile kimbululambulula litakutokea puani. Pigeni mdogomdogo au kitorondo watu wangu wa nguvu la sivyo mtajikuta kwa masnichi wa difenda. Dheni tuanze kuhaha kukuchomoa nyuma ya nondo! Acheni hizo!
Nimekuwa na sistimu ya kuwasanua wana kuwa taimu inamuvu fasta kinoma na ukweli wa yestadei unaweza kuwa uongo mkubwa kinoma wa tudei. Tunaanza kitu cha mwaka. Hapa sasa natoku na masela wangu wa kitaa. Wale tunaohaso pamoko na kutanua kwa mkwanja halali. Wale tunaosafa kinoma na hili laifu tukiwa apache alolo tumecharara.
Achana na dili fekelo za magumashi. Unajua ukiwa na ngawira au mawe ambayo umefaindi bila magumashi hata matumizi yake huwa hayana kabisa mastresi. Sasa wewe umetafuta mkwanja halafu unatumia kwa kujificha kama mafisadi si haina utamu mazee?
Ebana wanangu mmeshajaza dayari zenu kwa mipango ya 2015? Yap! Huo ndo mpango usije ukapelekwapelekwa kama ling’ombe bila maplani. Kichwa timamu hakiendiendi tu bila daireksheni. Sasa si dayari ndo fomula au taimu tebo? Kama bado sanuka wewe. Dunia ipo spidi unaachwa dakika ziro.
Kuna wanangu walizijaza hizo dayari lasti yia bati mambo hayakwenda poa so kama mudi zipo dauni hivi.
Ngoja nikupe sampo ya washikaji zangu walichokifanya na nini kilihapeni kwao.Wakati tukitafakari ishu zetu na jinsi ya kuliwini hili laifu, nikachati na vichwa vyangu vya longi.

Wanaampilifai kwamba kwa longi taimu wamegundua hakuna matokeo ya mwisho yanayofanana katika kutafuta kuliwini hili laifu.Katika mbio zetu wanangu tofauti na kila kichwa kinajua kitawini vipi kwa taimu gani. So usije ukagandamizia kila kitu. Kwanza prezidaa mzazi jembe alishasema akili za kuambiwa miksi na zako!
Sampo ni kwamba sela wangu ana eji ya miaka 30 dheni amefinishi kitu cha chuo kikuu kabisa bati tupo naye kwa kitaa anakula tu ugumu. Yaani yupo jobulesi. Wakati kuna dogo wa eji ya miaka 20 tu naye kachukua jiwe hapo chuo dheni tayari ana maisha kama ya waziri. Jamani huku si ni kuzinguana?
Achana na mfano huo, kuna shori anamaliza tu mastadi anapata mchumba na kuolewa akiwa bado na usichana wake. Kuna mwingine anamaliza skuli dheni anahaso kitaa, anatoa mimba kibwena na hapati jamaa wa kumuoa bati wote wanataka wafike pamoko mwisho wa laifu. Makubwa!
Cheki tena hii, masela wanajiuliza mshikaji anakuwa mkurugenzi kitambi meneja akiwa na umri wa miaka 20 dheni anakata ringi akiwa na eji ya miaka 50.Halafu kichwa kingine kinakula ubigi bosi kikiwa na eji ya miaka 40 dheni anadedi akiwa na eji ya 45. Hapo ni feya jamani?
Wanangu jipangeni wala hakuna kukata tamaa kozi spidi yako tu ndo itakutoa mapema. Weka silaha zako freshi kwa ajili ya 2015 ili neksti sizoni kama hivi tupeane marizalti tukiwa hepi mwishoni. Oya cha msingi kachaa usikate tamaa kaza jombaa kitaeleweka tu. Ama nini machalii wangu.
Tudei hakuna ngendembwe. Ngoja nitumie chansi hii kuwapa sharauti wanangu wote fromu kila chobingo tuliokuwa hapa jamvini lasti yia. Tuwe pamoko tena mwaka huu. Tupeane chalenji za namna na jinsi gani tutawini katika laifu hili.
Ebana eee…nawawishi mwaka mpya wa 2015 wenye mafanikio kibwena. Kwa mizinguo kitaa usiache kunibonyezea kwenye foni hapo juu dheni unipe mastori moo nami nitayarusha kwa mahewa.
Ebana sasa bata ndefu wapi maana nipo kifali zaidi soo kama vipi sii yuu neksti wiki.


Post a Comment

Previous Post Next Post