Polisi nchini Ufaransa wameendelea na msako wa washukiwa wanaotuhumiwa kuwaua wafanyakazi wa gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Msako
huo umeelekezwa zaidi katika jiji la Paris hasa katika mji wa
Picardy,ulioko upande wa Kaskazini Mashariki mwa jiji la Paris.
Ulinzi umeimarishwa pia katika kijiji cha Longpont, ambapo msako unaendeshwa nyumba kwa nyumba ambao unaambatana na upekuzi.
Waziri
wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, ameeleza kuwa askari
elfu themanini na nane wakiwemo maafisa wa ngazi za juu na askari wa
kawaida wanashiriki katika msako huo na kwamba wametawanywa kila pembe
ya jiji la Paris na vitongoji vyake tangu shambulio hilo litokee
Jumatano.
Mapema jana wanaume wawili waliokuwa na silaha,
wanaoaminika kuwa ni watuhumiwa wanaosakwa walivamia kituo kimoja cha
mafuta, na kuna wasiwasi kwamba watuhumiwa hao wawili huenda wakarejea
katika jiji hilo la Paris.
Ikiwa ni siku ya pili mfululizo maelfu
ya wananchi wa jiji la Paris wamefanya ibada katika eneo la Place de la
Republique kwa ajili ya kuwaombea watu kumi na wawili waliouawa kwenye
shambulio la Charlie Hebdo. Taa za mnara wa Eiffel zilizimwa mwishoni
mwa siku ya maombolezo. Mjini New York, wajumbe wa Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa walisimama kwa muda kuwakumbuka waathrika wa shambulio
hilo.



























Post a Comment