Kocha mpya wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
IMEBAINIKA kuwa uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa mechi tatu kwa benchi lake la ufundi linaloongozwa na Kocha Hans van Der Pluijm kisha ndipo litatoa tathmini juu ya mwenendo wa timu hiyo.Wakati kocha huyo akipewa mechi tatu na uongozi wake, yeye mwenyewe amezungumzia imani za kishirikina na kudai kuwa zinachangia kulimaliza soka la Afrika.
Kuhusu mpango wa mechi tatu ni kuwa hakuna mkakati wa kuangalia ajira ya kocha huyo kama anafaa au hafai kuendelea kuinoa Yanga kwa sasa lakini mechi ambazo ni kipimo kwake ni zile za Ligi Kuu Bara.
Awali kuliibuka tetesi kuwa Yanga inaweza kuanza kujiuliza juu ya kocha huyo baada ya kufungwa bao 1-0 na JKU katika robo fainali ya Kombe la Mapinduzi, juzi Alhamisi.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Yanga, Jerry Murro, alifunguka kwa kusema kuwa michuano hiyo kwao ilikuwa kama sehemu ya mazoezi kujiandaa na mashindano ya kimataifa na ligi kuu ambayo inaendelea.
Amesema kuwa uongozi ulipanga kutoa tathmini yake kwa benchi la ufundi baada ya mechi tatu za ligi kuu, ambazo ni dhidi ya Azam iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2, Mbeya City na Coastal Union ambazo bado hazijachezwa.
“Sisi tulipanga kutoa mechi tatu kwa kocha kabla ya kufanya tathmini ya mwenendo wa timu. Hivyo hakukuwa na sababu ya kufanyia tathmini michuano ya Mapinduzi kama wengi wanavyozusha,” alisema Murro.
Kuhusu ushirikina, kocha huyo ambaye anifundisha Yanga kwa mara ya pili, alisema kuwa tangu aanze kufundisha soka miaka 19 iliyopita, hajawahi kushuhudia kitendo cha kishirikina katika soka kama ilivyotokea hivi karibuni katika mchezo wao dhidi ya Shaba.
Jumanne iliyopita, shabiki wa Yanga maarufu kwa jina la Carlos, aliingia uwanjani pembeni ya lango la wapinzani na kuchukua glovu za akiba za kipa wa Shaba, Bakari Shaweji kisha kukimbia nazo ikiwa ni katika dakika ya 81, ambapo dakika tano baadaye Andrey Coutinho aliifungia Yanga bao zuri.
Akizungumza na Championi Jumamosi, kocha huyo alifunguka kuwa tangu aanze kufundisha mwaka 1996 barani Afrika tukio hilo lilimshangaza zaidi.“Mambo ya kishirikina yanachangia soka la Afrika kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa na kupoteza saikolojia ya wachezaji uwanjani, hasa tukio linapotokea mpira ukiwa unaendelea uwanjani si vyema sana,” alisema Pluijm

Post a Comment