Kuwapo kwa kundi la vijana wanaofanya uhalifu
maarufu kama ‘Panya Road’ ambao wamekuwa wakipora na kujeruhi watu
katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, kumegeuka kama mchezo
wa kuigiza kwa Jeshi la Polisi ambalo limetangaza kuwatia mbaroni
watuhumiwa 510.
Hatua ya polisi kufanya msako wa kundi hilo la kihalifu ilitokana na malalamiko ya wananchi dhidi ya Jeshi hilo kutokana na kupewa taarifa za tukio la Ijumaa la kupora na kupiga watu katika maeneo kadhaa ya Wilaya ya Kinondoni, lakini wakakana kuwapo kwa kundi hilo.
Hatua ya jeshi hilo kuibuka na kuanzisha operesheni dhidi ya watuhumiwa hao hakuna tofauti na mchezo wa kuigiza kwa sababu kabla ya kikundi hicho kusambaa, polisi walikuwa na taarifa lakini hawakuchukua hatua na badala yake walibeza suala hilo.
KAULI ZA KOVA
Jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari, alisema vijana 510 pamoja na viongozi wao watatu wa kundi hilo, wametiwa mbaroni.
Alisema kukamatwa kwa kundi hilo kumefuatia operesheni iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Kamishna Kova alisema vijana hao waliokamatwa wamehusishwa na kundi hilo ni pamoja na wapiga debe katika vituo vya daladala, wacheza kamari na vijana wanaokaa katika vijiwe huku wengine wakikamatwa katika msako wa nyumba kwa nyumba na kukutwa na familia zao.
Alisema katika msako huo, jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata vijana ambao wanasadikika ni viongozi vinara wa kundi la Panya Road na kuwataja kwa majina.
Hata hivyo, majina ya vinara hao kwa sasa tunayahifadhi ingawa Kova alisema ni wakazi wa Tandale Sokoni na Mburahati kwa Jongo.
Kamishna Kova aliongeza kuwa upelelezi dhidi ya watuhumiwa hao unaendelea na kwamba hakuna mtuhumiwa yeyote atakayewawekea dhamana na kuwataka ndugu au wazazi wa watuhumiwa hao wasifike katika vituo vya polisi kwa lengo la kuwawekea dhamana.
Alisema makamanda wa mikoa ya kipolisi ya Ilala, Kinondoni na Temeke, wanasimamia wenyewe operesheni ya kuwasaka na kuwakamata vijana hao popote walipo ili sheria ichukue mkondo wake.
Kamshina Kova alisema Jeshi hilo lina mpango wa kushirikiana na watendaji ngazi ya mitaa, kata, tarafa na wananchi kwa ujumla kufanya mikutano ili kuwabaini wahalifu au makundi ya uhalifu katika maeneo yao.
Aidha, Kamishina Kova alitolea ufafanuzi juu ya taarifa za awali alizozitoa katika vyombo vya habari kuwa hakukuwa na tukio lolote la uvunjifu wa amani lililokuwa likifanywa na kundi la kihalifu la Panya Road.
Alisema kuwa tukio hilo halikuwa kubwa kiasi cha kuleta hofu kubwa kwa wananchi kwani Jeshi la Polisi lilikuwa limejipanga kikamilifu, hivyo taarifa hizo zilichochewa na mitandao ya kijamii, madereva wa bodaboda na wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii kama Whatsap na Facebook.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, kuliibuka taharuki, hofu na wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kundi la Panya Road kuvamia mitaa mbalimbali na kupora mali.
Baadhi ya maeneo ambako kundi hilo linadaiwa kufanya uporaji ni Kagera, Magomeni,Tabata, Sinza, Mwananyamala, Kinondoni, Kijitonyama, Manzese, Kigogo na Buguruni.
KAULI TATA ZA POLISI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam mara kadhaa kunapotokea matukio makubwa, limekuwa likitoa kauli ambazo wakati mwingine huwa tata na kuonekana kama mchezo wa kuigiza.
Mfano ni tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Stephen Ulimboka, Juni, 2012.
Jeshi hilo lilimkamata raia wa Kenya, Joshua Mulundi, likidai kuwa alitubu katika Kanisa la Ufufuo na Uzima la Mchungaji Josephat Gwajima, kuwa ndiye aliyemdhulu Dk. Ulimboka.
Hata hivyo, baada ya siku mbili, Mchungaji Gwajima alitoa taarifa za kukanusha mtu huyo kwenda kutubu kanisani kwake.
Pia Mahakama ya Kisutu, ilimfutia mashitaka na kumwachia huru baada ya kuonekana hana kosa. Hata hivyo, alitozwa faini ya Sh. 1,000 kwa kosa la kuwadanganya polisi kuwa alihusika kumteka Dk. Ulimboka.
Jeshi hilo pia liliwahi kutoa picha za mtu ambaye lilidai kuwa ndiye aliyechukua kompyuta mgando (laptop) ya marehemu Dk. Sengondo Mvungi, baada ya kuuawa mwaka jana.
Hata hivyo, hadi leo Jeshi hilo halijamkamata wala kueleza kuhusu upelelezi ulipofikia.

Post a Comment