Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya
madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani
vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi
karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40
jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo
yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi
itakapojengwa upya. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA
MATUKIO BLOG
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa
hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua
viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.
Watioto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa
Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za
mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea
mnara
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma,
Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi kuboresha barabara na mawasiliano ya
simu
Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji
cha Kwa Mduma wakati wa ziara yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata
ya Kibindu
Post a Comment