Waziri wa uchukuzi Dokta Harrison Mwakyembe ameuagiza uongozi wa
kiwanja cha ndege cha nduli mkoani Iringa pamoja na uongozi wa mkoa huo
kubainisha mipaka ya kiwanja hicho cha ndege kwa lengo la kutambua
nyumba zitakazoathirika na zoezi la upanuzi wa kiwanja hicho.
Dokta Mwakyembe ametoa agizo hilo mara baada ya kukagua kiwanja
hicho nakusema kuwa wananchi wanaoishi katika eneo la kuzunguka kiwanja
wanapaswa kushirikiana na serikali katika kumaliza changamto zinazoweza
kujitokeza katika kutekeleza mradi huo.
Katika taarifa yake kwa waziri huyo meneja wa kiwanja cha ndege cha
nduli Hanna Kibopile amesema kiwanja hicho kinakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo gari la zimamoto,uchakavu wa miundombinu pamoja na
uvamizi wa wananchi waliojenga ndani ya eneo la kiwanja.
Kufuatia agizo hilo la waziri Mwakyembe mkuu wa mkoa wa Iringa
Amina Masenza ametoa wiki mbili kwa mkurugenzi wa halmashauri ya
manispaa ya Iringa kufanya zoezi hilo la utambuzi wa waliovamia na
kujenga ndani ya kiwanja hicho.

Post a Comment