Simba
SC ya Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya
kufunga Mtibwa ya Turiani, Morogoro kwa mikwaju ya penalti katika mchezo
mkali uliofanyika Uwanja wa Aman, Zanzibar.
Hatua
hiyo ya mikwaju ya penalti ilikuwa baada ya timu hizo kutoshana nguvu
0-0 katika dakika 90 za kawaida ambapo kwa mujibu wa taratibu za
michuano hiyo, hakuna dakika 30 za nyongeza iwapo timu zitatoka sare.
Simba
ilipata penalti nne huku Mtibwa ikipata penalti 3, kila kipa akipangua
mkwaju mmoja, wakati penalti nyingine ya Mtibwa ikigonga mwamba.
Kipa
Ivo Mapunda wa Simba aliyeingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya mlinda
mlango kinda Manyika Peter, ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kupangua
penalti ya mwisho ya Mtibwa iliyopigwa na Vicent Barnabas.

Post a Comment