Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe (Mb) ameondoka nchini tarehe 13 Januari 2015 kwenda Urusi kwa
ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Urusi, Mhe. Sergey Lavrov.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
Mhe. Membe anatarajiwa kutumiafursa hiyo kuhimiza ushirikiano wa
kiuchumi na Urusi, hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na
ubadilishanaji wa teknolojia. Tanzania inaweza kufaidika na utaalamu wa
Urusi katika sekta za uzalishaji wa nishati, uvuvi, afya, kilimo na
huduma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Tarehe 14 Januari, 2015.
Post a Comment