JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwaarifu
Wizara imeanza zoezi la kuwapangia vituo vya vya kazi Wataalam wa Kada
za Afya kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Wataalam wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kwa waajiri wao
ndani ya siku 14 tangu tarehe ya tangazo. Aidha,waajiri wanakumbushwa
kuwasilisha taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
kuhusu wataalam ambaohawajaripoti ili kuona uwezekano wa kujaza nafasi
zao.
Vilevile, waajiri wanakumbushwa kukagua vyeti halisi vya kidato cha IV
na VI, Vyeti vya taaluma na vyeti vya usajili (kwa wataalam wenye
masharti ya usajili kwa mujibu wa miundo yao yau tumishi).
Orodha ya majina ya wataalam waliopangiwa kazi pamoja vituowalivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa awali.
Nawapongeza wataalam wote kwa kupata nafasi ya kutumia utaalam wenu
katika kuwahudumiwa wananchi, na ninawatakia kazi njema na utumishi
uliotukuka.
Imetolewa na:-
Katibu Mkuu
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
06 Januari, 2015
Post a Comment