Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wamesema hatua zinazochukuliwa na
serikali dhidi ya viongozi waliohusika na kashifa ya akaunti ya Tegeta
Escrow hairidhishi na kuahidi kupambana ili haki itendeke kwa maslahi
ya watanzania.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR mageuzi Mh.James Mbatia ameyasema hayo
wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la vunjo katika mkutano wa
hadhara na kusema kuwa tatizo la ufisada unaofanywa na viongozi wachache
wa serikali limesababisha nchi kuyumba.
Amesema kwa pamoja vyama hivyo havijaridhishwa na hatua
zinazochukuliwa dhidi ya viongozi husika kwa madai kuwa serikali
inajichanganya kuhusu sakata hilo na kwamba bunge ndilo litakalomaliza
mzozo huo kwa maslahi ya wananchi.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Mh.Joshua
Nasar amesema umoja huo utahakikisha haki inatendeka kwa maslahi ya
watanzania kwa madai kuwa nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali
katika sekata ya elimu afya na ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wapo
watu wachache wanaonufaika na kodi za watanzania.
- ITV
Post a Comment