Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi David Kafulila amesema kama upinzani utashindwa kuchukua nchi mwaka huu,basi CCM itaendelea milele kuongoza Tanzania.
Oktoba mwaka huu Tanzania inaingia kwenye kinyang’anyiro cha cha
uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani baada ya Rais Kikwete kumaliza muda
wake.
Kafulila alisema Watanzania watendelea kubaki maskini huku keki ya Taifa ikiliwa na vigogo wachache.
“Huu ni wakati wa kuajingalia…watu wanalalamika kila siku,hali ya
umaskini inaongezeka na kila kukicha ni kilio,sasa ni wakati wa kufanya
uamuzi”alisema Kafulila.
Alisema umaskini wa Mtanzania unachangiwa kwa kiasi kikubwa na wezi
wa rasilimali za nchi,huku Watanzania walio wengi wakitaabika.
“Mimi nasema upinzani ukiingia Ikulu haya yote yatamalizika,kila
Mtanzania atafurahi rasilimali zake,lakini waking’ang’ania CCM watabakia
hivyo”alisema.
Alisema ikiwa watashindwa kuitoa CCM na ikafanya vizuri katika kila
eneo,Watanzania hasa wapinzani watabaki kwenye uongozi wa mitaa,vijiji
na vitongoji walivyopata katika uchaguzi uliopita kwa miaka mitano
mingine.
Post a Comment