VIDEO:- WAISLAM, WAKRISTO WAFANYA KONGAMANO LA AMANI

Katibu Mkuu wa Jopo la Mashehe Tanzania, Sheikh Hamis Mtaka akihutubia.
Askofu wa EAGT, Philbert Mbepera akisisitiza jambo.
Sheikh Hemed Jalala wa Msikiti wa Kigogo Post akizungumzia amani.
Mwenyekiti wa Imam Bukhary Islami Foundation,  Khalifa Hamis.
Baadhi ya waumini wa Kiislamu na Kikristo wakiwa katika kongamano hilo.
Sehemu ya meza kuu, juu ni ujumbe wa kongamano hilo.
IMAM Buhkary Islamic foundation leo imefanya kongamano la amani kwa kuwashirikisha maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya kikristo.
Kongamano hilo linalofanyikia Hotel ya Lamada, jijini Dar es Salaam limeanza leo na litamalizika kesho, limelenga kudumisha upendo na amani kwa waumini wa madhebu yote nchini.
Katibu Mkuu wa Jopo la Mashehe Tanzania, Sheikh Hamis Mtaka alisema: “Uislam kama dini hauna tatizo na Ukristo, kwa sababu Mwislamu anautambua Ukristo na ukristo unautambua Uislam. Ambaye hautambui Uislam au Ukristo huyo anaitikadi yake binafsi na anataka kutumia dini kama kigezo cha kufanya mambo yake…tusimruhusu.”

Post a Comment

Previous Post Next Post