Na RFI
Wataalamu wa kimataifa, hata hivyo, wamesema hawajaweza kuviondoa kutoka
chini ya bahari kwa sababu vimekwama kati ya vipande viwili vya ndege
hiyo.
Wizara ya uchukuzi ya Indonesia imesema, leo Jumatatu kuwa watalaamu hao
wanatarajiwa kukiondoa majini kipande cha ndege hiyo kwa kutumia mifuko
maalum ya majini na kuviondoa visanduku hivyo.
Maafisa wanaamini kuwa wahanga wengi wa ajali hiyo bado wamekwama ndani
ya kipande cha katikati cha ndege hiyo. Jumapili Januari 11, kipande cha
mkia kiliondolewa majini lakini wataalamu hawakupata visanduku hivyo
vya kurekodi mawasiliano.
Kufikia sasa miili 48 kati ya watu 162 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo imepatikana.
Post a Comment