Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin
Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa
uzinduzi wa Promosheni mpya inayojulikana kama JayMillions
itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali
zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja
anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila
siku.Kushoto ni Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia
ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Balozi
wa promosheni ya JayMilions Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)akionesha
bango linaloelezea jinsi ya mteja kujua kama ameshinda katika Promosheni
hiyo iliyozinduliwa na Vodacom Tanzania leo itakayowawezesha wateja wa
kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi
Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu
kila siku yenye neno “JAY” kwenda namba 15544.Wengine kutoka kulia
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Mkuu wa
Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin
Twissa(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya inayojulikana kama
JayMillions itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi
mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama
umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda
namba 15544 kila siku.Kushoto ni Balozi wa promosheni hiyo Hilary
Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo
Matina Nkurlu.
Mkuu
wa Kitengo cha huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania, Saurabh
Jaiswal(kushoto)akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa
kampuni hiyo,Kelvin Twissa(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya
inayojulikana kama JayMillions itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo
kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili
kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno
“JAY” kwenda namba 15544 kila siku.Katikati ni Balozi wa promosheni hiyo
Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni
hiyo Matina Nkurlu.
Dar es Salaam, Tanzania, Januari 13, 2015:
Vodacom imezindua promosheni kubwa kuliko zote katika historia ya
michezo ya bahati nasibu nchini Tanzania ambapo wateja watajishindia
pesa taslimu Sh. bilioni 30/- katika zawadi ndani ya kipindi cha siku
100.
Akizungumza na waandishi wa habari jjijini
leo ,Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema promosheni
hii inajulikana kama JayMillions na inawahusisha wateja wote wa Vodacom
na ni ya kwanza ya aina yake kwani, “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa
kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”
Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-,
washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi mia moja wa Sh. 1m/- KILA SIKU
kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa
bure wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku.
Meza ameongeza kuwa hii inadhihirisha
dhamira ya kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia
ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi “ambao
wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na
Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema ili kushiriki katika promosheni
hii, mteja yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma
SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama
ameshinda au la. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe
mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo
atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS
itagharimu Sh. 300/- tu.
“”Tofauti na promosheni zilizopita,
JayMillions ni rahisi sana kushiriki. Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara
moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi, wala chemsha bongo na hivyo
kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi kwa wateja wengi kuibuka
washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku unatuma ujumbe mfupi,”
alieleza Twissa.
Alisema kila siku namba zilizoshinda
zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii. “Ili kujua kama
namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda kukusisitizia mteja wetu kutuma
ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda 15544 ili wasipoteze bahati zao
iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza
kupoteza mamilioni kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa
kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku,” alisisitiza Twissa.

Post a Comment