Mahakama nchini misri imebatilisha
uamuzi wake kuhusiana na tuhuma za uproraji wa mali ya umma zilizokuwa
zinamkabili aliyekuwa Rais wa wa nchi hio, Hosni Mubarak, na wanawe
wawili.
Mahakama hio sasa inasema kesi hio itaanza kusikilizwa
upya. Mahakama imemeelezea kuwa imegundua mikakati ya kisheria
haikufuatwa.
Uamuzi huo una maana kwamba Mubarak ataondolewa
katika hospitali ya kijeshi ambako anazuiliwa kwa mujibu wa wakili wake.
Hio ndio kesi iliyoyokuwa imesalia mahakamani dhidi yake.
Mnamo
mwezi Mei mwezi jana, Mubarak alikuwa emehukumiwa jela miaka mitatu kwa
kupora mamilioni ya dola pesa ambazo zilinuiwa kuikarabati ikulu ya
Rais.
Wanawe Mubarak, Gamal na Alaa,walifungwa jela miaka minne wakati hukumu ilipotolewa dhidi ya babao.
Tuhuma
nyinginezo dhidi ya Mubarak ya kuamrisha mauaji ya waandamanaji mwaka
2011 wakati wa mapinduzi ya kiraia, zilitupiliwa mbali mwezi Novemba
mwaka jana(BBC)

Post a Comment