Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla ameuagiza uongozi wa Bodi ya Kampuni ya Maji Safi na Majitaka
Dar es Salaam (Dawasco), kuwaondoa mameneja wawili wa kampuni hiyo
kutokana na wizi wa maji kufanyika kwenye maeneo yao.
Makalla amesema udhaifu unaofanywa na watendaji wa
Dawasco unasababisha malalamiko mengi kwa wananchi. Alisema hayo jana
wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya katika mamlaka hiyo huku
akiagiza mameneja hao, Robert Mugabe wa Boko na Peter Chacha wa Kimara
Temboni kuondolewa.
Katika maeneo aliyoyatembelea ya Magomeni Kagera,
Kimara Temboni na Boko alishuhudia mitandao ya maji ya wizi ikiwa
imefungwa maeneo ya wazi na vichochoroni.
“Kinachosikitisha zaidi ni kutokuwa na utaratibu
wa kutoa taarifa kwa wananchi maji yanapokosekana, siwezi kuikubali hali
hii. Jana tumekamata wezi 12, nimeagiza wawatafute wengine wakatwe,”
alisema Makalla.
Post a Comment