Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu
**
OFISA Mtendaji wa kijiji cha Lumesule, Kata ya Lumesule, wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, Swalehe Daimu, anadaiwa kupigwa na mkazi wa kijiji hicho, kwa madai ya kumkamata dada yake na kumtoza faini ya Sh 5,000 kwa kushindwa kushiriki shughuli za ujenzi wa maabara.
Kutokana
na hatua hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego, ambaye yupo ziara
ya ukaguzi wa maabara katika wilaya hiyo, alimwagiza Mkuu wa wa Wilaya
kukamatwa haraka kwa mtuhumiwa huyo na kumfikisha mahakamani
**
OFISA Mtendaji wa kijiji cha Lumesule, Kata ya Lumesule, wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, Swalehe Daimu, anadaiwa kupigwa na mkazi wa kijiji hicho, kwa madai ya kumkamata dada yake na kumtoza faini ya Sh 5,000 kwa kushindwa kushiriki shughuli za ujenzi wa maabara.
Akizungumza
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu, kijijini hapo jana,
mlinzi huyo wa amani alisema kuwa tukio hilo limetokea Februari 4 mwaka
huu, baada ya kuwakamata watu kumi kijijini hapo ambao hawakushiriki
katika ujenzi wa maabara zinazoendelea kujengwa katika shule ya
sekondari Lumesule.
“Sisi
kama kijiji tumetunga sheria ndogo za usimamizi wa ujenzi huu, na
mwananchi yeyote ambaye hakushiriki ni lazima akamatwe na kisha atozwe
kiasi hicho cha fedha ili zisaidie kuendeleza ujenzi,” alisema.
”Baada
ya kuwa nimewashikilia hawa watu na kuwafungia katika ghala la kijiji,
huyo bwana alikuja kwa ajili ya kumlipia ndugu yake faini hiyo na kisha
kunipiga vibao na kisha kunitishia maisha,” alifafanua Daimu.
Kwa
mujibu wa mtendaji huyo, mtuhumiwa huyo amekuwa kikwazo kikubwa kwa
shughuli za maendeleo kijijini hapo kwa kuwashawishi wananchi
kutoshiriki shughuli za ujenzi wa maabara na miradi mingine ya
maendeleo.
Akieleza
tukio hilo, Daimu alilitupia lawama Jeshi la Polisi kwa kushindwa
kumkamata mtuhumiwa licha ya kutoa taarifa kituo kikuu cha Polisi cha
wilaya Mangaka, na kwamba mpaka sasa mtuhumiwa huyo yupo kijijini hapo ,
anaendelea kuwashawishi wananchi kukataa kushiriki ujenzi huo.
Post a Comment