Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Bunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo |
Chama cha wananchi CUF leo kimetangaza rasmi kuanza
kwa mchakato wa kura ya maoni kwa ajili
ya kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chama katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu,ambapo zoezi la kutoa form kwa
wanachama wake wanaotaka nafasi mbalimbali kama nafasi ya madiwani,ubunge na
pia nafasi ya urais wa Tanzania zimeanza kutolewa EXAUD MTEI ANAKUPA STORY YOTE
Akizungumza Kuanza kwa zoezi hilo mkurugenzi wa
orgazation na uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo, amesema
kuwa kwa sasa milango iko wazi kwa mwanachama yeyote mwenye sifa za kugombea
uongozi ndani ya chama hicho kijitokeza kuchukua form kwani ni nafasi ya
kipekee ya kuonyesha democrasia ndani ya chama hicho.
Akitaja gharama za kuchukua form ya kugombea nafasi
mbalimbali amesema kuwa nafasi ya udiwani gharama ya form ni 10,000,nafasi ya
ubunge ni 50,000 huku mgombea wa nafasi ya urais atachukua form kwa gharama ya
shilingi laki tano.
Mketo Amesema
kuwa kuanza kwa zoezi hilo ndani ya chama haina maana kuwa ni kukiuka
makubaliano umoja wa katiba ya wananchi UKAWA bali walichokubaliana ni kuwa
kila mwanachama ahakikishe anatafuta wagombea wake na kisha kuwaweka pamoja
kuangalia ni nani anafaa kuwa mgombea na kwa nafasi gani hivyo wananchi wasiwe
na wasiwasi kuhusu umoja huo kwani bado upo
imara na hauyumbi.
Katika hatua
nyingine chama cha wanachi cuf kimealamikia kuchezewa rafu na viongozi wa
serikali kwa kulitumia jeshi la polisi vibaya ambapo amesema kuwa kuna baadhi
wa viongozi wake wa mikoani ambao wamekuwa wakikamatwa na polisi na ndani kwa
kile kinachoitwa ni kujihusisha na vitendo vya ugaidi ambapo amesema kuwa hizo
ni mbinu chafu za kuwaponguza kasi viongozi hao baada ya kuona kuna uwezekano
wa wao kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na wanaweza kushinda nafasi
hizo,majina ya viongozi hao waliokamatwa nimekuwekea mwisho wa story hii mdau
wangu
TAMKO NZIMA HAPA
Post a Comment