Flaviana Matata, Miss Tanzania Liliani Kamazima na msanii T.I.D, Wamesikika Leo Katika 255 February 12

 Sikiliza 255 ya leo February 12, kutoka kwenye show ya XXL ya Clouds Fm na story ya kwanza kusikika inamhusu mwanamitindo Flaviana Matata ambapo mratibu wake amezungumzia ishu ya ile kampeni iliyokuwa inafanywa na  Flaviana Matata Foundation ya kuchangia vifaa vya kujenga Shule ya msingi Msinune iliyoko Bagamoyo, amesema baadhi ya michango imeshakamilika na miezi michache ijayo michango hiyo yakiwemo madawati vitakabiziwa kwenye Shule hiyo.
 Baada ya shindano la Miss Tanzania kufungiwa watu wengi wamekuwa wakijiuliza endapo mshindi wa mwaka huu atashiriki katika mashindano ya Miss World mwakani ambapo Miss Tanzania 2014, Liliani Kamazima amesema kuwa atashiriki kama kawaida ingawa hajui miaka miwili iliyobaki na kuhusu kufungiwa kwa mashindano hayo amesema hatua hiyo imeziba ndoto za wasichana waliotaka kushiriki.
Kwenye 255 ya jana mwanamziki Q Chief alizungumzia ishu ya msanii T.I.D  kumlaumu kuwa yeye ndio chanzo cha Top Bad kufa, na kukanusha vikali na kumtupia lawama T.I.D, kwenye 255 ya leo msanii T.I.D amesema kuwa ameamua kuto kuzungumza chochote juu ya jambo hilo na kusikitishwa na maelezo ya Q Chief  kwa kuwa alizungumza ukweli na kwa sasa amenunua vyombo vingine na Top Band iko pale pale.
Sikiliza 255 yote hapa kwa kubonyeza play hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post