Kionjo cha video mpya ya Madee alichokitoa online cha video yake mpya ‘Vuvula’ anayotarajia kuizindua Jumamosi hii pale Escape One, kimewapa wasiwasi mashabiki kama itakubaliwa kurushwa na TV za nyumbani endapo video itabaki kuwa hivyo.
Katika ‘teaser’ ya video hiyo iliyoongozwa na AJ wa Next Level, kuna msichana ambaye anacheza nusu uchi.
Madee ameiambia Bongo 5 kuwa kutakuwa na version safi isiyo na vipande hivyo, ambayo ndio itakayosambazwa kwenye vituo vya TV vya nyumbani.
“Ile video haijatoka unajua watu wanajaribu tu kuanza kujudge mapema, video haijatoka inatoka tarehe saba hiyo ni teaser “. Amesema Madee.
“Halafu sasa kingine mi sioni kama kuna tatizo lolote kwa sababu ile ni teaser tu imetoka kwenye social network sio kwenye media, inamaana mtu ana simu yake ana computer yake anakaa nyumbani anaangalia, mbona kwenye simu kuna vitu kibao tu watu wanaangalia vikubwa tu, sio kwamba imeshatolewa imewekwa kwenye TV yako nyumbani.”
Hizi ni baadhi ya comments kuhusiana na ‘teaser’ hiyo.
Michael Minja:
Hii video ni bora aifanyie marekebisho mapema kabla hajaitoa kwa maana haita weza kuchezwa lazima itafungiwa haina maadili.
classic_philip:
Hata wakifungia youtube ipo kwenye library zitakuwepo tutaangalia tu kwanza siku hizi watu hawana mda wa kukaa eti waangalie tv
makama_jr:
@babutale mmezngua. U can’t release a such kind of video. Lol huo ni uzalilishaji wa wanawake.
Post a Comment