MALICK: SIJAONA KAMA ROSE NDAUKA WA KUNITETEMESHA



MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe ambaye sasa anatamba na wimbo wake wa Tucheze amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa tangu atengane na mzazi mwenziye, Rose Ndauka bado hajatokea wa kumtetemesha.


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Malick Bandawe.

Akizungumza na juzikati, Malick alisema kuwa huko nyuma alipomuona Rose alimtetemesha na kuamua kuingia mzimamzima mpaka kufikia hatua ya kupata naye mtoto lakini mpaka sasa hajatokea kama yeye.

“Unajua mambo yanapotokea lazima kukubaliana nayo na huwezi kulazimisha. Tangu uhusiano wetu usambaratike, hajatokea kama Rose,” alisema Malick

Post a Comment

Previous Post Next Post