ONESHO
la burudani ya warembo lililoitwa Miss Valentine, lililofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Vybe mjini hapa
kusherehekea siku hiyo ya wapendanao, liligeuka kuwa kichefuchefu mbele
ya aliyekuwa mgeni rasmi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.
Mrembo akipita jukwaani katika onesho la burudani ya warembo lililoitwa Miss Valentine huko Morogoro.
Mmoja wa warembo walioshiriki onesho hilo, ambaye jina lake
halikupatikana mara moja, alipita jukwaani akiwa amevalia nusu utupu,
hali iliyosababisha mamia ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo
kumzomea kwa sauti kubwa.
Zomeazomea hiyo ilimshtua mwandaaji wa onesho hilo, Alex Nikitasi ambaye alipanda jukwaani na kumkinga msichana huyo asipigwe picha na mwandishi wa gazeti hili, kabla ya kumtolea maneno ya dhihaka.
Zomeazomea hiyo ilimshtua mwandaaji wa onesho hilo, Alex Nikitasi ambaye alipanda jukwaani na kumkinga msichana huyo asipigwe picha na mwandishi wa gazeti hili, kabla ya kumtolea maneno ya dhihaka.
Nikitasi ambaye pia ni mwandaaji wa Shindano la Redds Miss Kanda ya
Mashariki kwa zaidi ya miaka mitano, alisikika akisema; We Shekidele
unataka kumtoa mrembo wangu kwenye magazeti yako ya udaku, sitaki umpige
picha.

Baadhi ya watu waliohudhuria onesho hilo walilaani kitendo cha mrembo
huyo kupita na vazi hilo na mwandaaji wake kumtetea, wakisema vitendo
kama hivyo vinashamiri kwa sababu wanaopaswa kuvidhibiti, wanavitetea.
Ingawa hakusema lolote, lakini Mstahiki Meya na wageni wengine wa
jukwaa kuu hawakuonesha kufurahishwa na kitendo hicho cha kukiukwa kwa
maadili waziwazi.
Post a Comment