Kuna michango ya fedha ambayo inaibuka mara kwa
mara hasa katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, mfano
tumechangishwa Sh 10,000 kwa ajili ya maabara, lakini juzi tena tumekuja
kuchangishwa Sh 3,000 ambayo tutatakiwa kulipa kila mwezi kwa ajili ya
ulinzi shirikishi hata kama una mlinzi unayemlipa, je, utatusaidiaje
kudhibiti michango ya namna hiyo.
Jibu: Suala hilo linadhibitiwa
kupitia vikao vya serikali za mtaa kwa kuwa ndiyo wanajadili na
kupitisha hayo hivyo wananchi washiriki mikutano ya serikali za mitaa na
kuhoji hayo. Mikutano hiyo huitishwa kila baada ya miezi miwili hivyo
wananchi wahudhurie kwa kuwa wengi hawahudhurii.
2. Yusuph Abdalah mkazi wa Darajani
Ni lini daraja la JKT njia panda ya Coca Cola Kawe litajengwa kwa kiwango cha zege ili kulifanya liwe imara?
Jibu: Kiujumla katika halmashauri
ya Kinondoni tumekuta kuna changamoto nyingi za utekelezaji wa miradi
ya maendeleo na hiyo ni kutokana na makusanyo madogo ya Sh8 bilioni
walizokuwa wanakusanya zamani kabla ya kuingia sisi. Katika fedha hizo
walikuwa wanatenga Sh1 bilioni kwa ajili ya maendeleo na pale kuna
majimbo matatu Kawe, Kinondoni na Ubungo. Hivi sasa tumefanikiwa
kufikisha makusanyo ya Sh37 bilioni na kati ya hizo Sh13 bilioni ni za
miradi ya maendeleo. Tumejenga barabara za lami mpya nne katika eneo la
Mikocheni Tumejenga daraja kubwa la Nyerere. Changamoto ya hilo la njia
panda tutalifanyia kazi katika mwaka huu wa fedha 2015/16, lakini
kinachotakiwa kufanyika ni wananchi kuhakikisha mwenyekiti wa mtaa wa
Mikocheni B kupeleka kwa WDC ili ipitie na kuileta kwenye vikao vya
halmashauri ambavyo mimi naingia ili tuweze kulishughulikia.
3. Godlove Jophrey mkazi wa Kawe.
Mimi ni miongoni mwa wananchi wengi wanaoishi Kawe
ambao tulipanda mbegu DEC, lakini mambo yaliyojitokeza yametufanya
wengi wetu tusijue hatima ya fedha zetu hadi leo, hivyo tumeyumba
kiuchumi. Utatusaidia vipi kujua hatma ya fedha zetu?
Jibu: Suala la DEC
tumelizungumzia na hivi sasa lipo mikononi mwa Serikali. Tumeomba
Serikali irudishe fedha hizo kwa wananchi na sisi kama watumishi tuna
mipaka yetu na hapo ndipo tulipofikia kwamba Serikali ndiyo inapaswa
kuzirudisha hizo fedha kwa wananchi.
4. Gaudence Manyanga mkazi Mzimuni.
Kawe Mzimuni na Ukwamani hakuna sehemu ya kutupia
taka hivyo kumekuwa na hali ya utupaji ovyo wa taka ambao unachafua
mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa maeneo hayo, unatusaidiaje
kupata eneo maalumu la kutupa taka?
Jibu: Eneo la kutupa taka ni
miongoni mwa mambo ambayo tayari tumelifanyia kazi, tumeshakaa na
watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa kutafuta eneo maalumu la
kutupa taka kwa eneo la Ukwamani na Mzimuni
Post a Comment