Wakati Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ukifikia hatua ya Kura
ya maoni inayotarajiwa kupigwa Aprili 30 mwaka huu, watu wameendelea
kutoa maoni yao.
Wapo wanaoamini kwamba, mchakato huo hautapita
kutokana na mambo kadhaa wanayoyaeleza na wengine wanaosema kuwa hawana
shaka na kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa katika kura ya maoni.
Mbunge wa Wawi (CUF), kisiwani Zanzibar, Hamad
Rashid Mohamed ni miongoni mwa watu wanaoamini kuwa Katiba
Inayopendekezwa itapita. Anasema hana shaka Katiba hiyo itapita hata
Zanzibar kutokana na maboresho mbalimbali yanayohusu kero za Muungano.
Anasema pamoja na kasoro nyingi zinazoelezwa,
Katiba Inayopendekezwa haina tatizo kubwa, hasa ikizingatiwa kuwa kuna
maeneo mengi yenye migororo baina ya Wazanzibari na Watanganyika,
yamefanyiwa kazi.
“Lakini pamoja na yote hayo nishukuru kwa hatua
iliyofikiwa. Ningeomba kwanza, vyombo vya habari vijaribu kueleza na
upande wa mazuri yaliyopitishwa kwenye rasimu hiyo...Kwa mfano suala la
mafuta ambalo lilishindikana kwa miaka mingi tangu enzi za Rais Hayati
Karume, lakini limewezekana sasa kwa Rais Dk Shein,” anaeleza.
Hamad anaeleza kuwa Katiba Inayopendekezwa
imeingiza mambo mengi ya msingi ambayo yalikuwa kilio cha Wazanzibari,
hivyo kustahili kupigiwa kura ya ndiyo, tofauti na madai ya wengi kwamba
haifai.
“Katiba imeingiza mambo yote ya msingi yaliyokuwa
yakipigiwa kelele na Wazanzibari. Wengine wanasema Katiba imevunjwa na
Zanzibar, lakini siyo kweli ifahamike kwamba yapo mambo yanayounganisha
kikatiba na mengine ni makubaliano,” anasema na kuongeza:
“Nitakupatia mfano, Cubeq waliingia kwenye kura ya
maoni mara sita sasa tangu walipohitaji kujitoa Canada, lakini
waliambulia asilimia 49, walipohojiwa tatizo nini? Wakasema tatizo ni
uwakilishi basi wakapewa nafasi ya kuiwakilisha Canada kupitia Unesco je
wamevunja Katiba?”
Anaendelea “Ni kama wanandoa, mambo mengi wanakubaliana ambayo ni kinyume na ndoa yao, je ndoa inakuwa imevunjika?”
Hamad anasema siyo kila kitu kinaweza kuingia
kwenye Katiba na hata madai ya Wazanzibari yatamalizwa kwa hatua.
Muungano ni damu siyo Katiba hebu angalia Watanganyika ambao ni asilimia
60 wanaoishi Zanzibar leo hii tukivunja Muungano tutawapeleka wapi?”
Kwa mujibu wa Hamad, Wazanzibari wanahitaji mikopo
na misaada bila vikwazo na kama hivyo vikipatikana, kilichobaki na
mambo ya utawala.
Anabainisha kwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba
ulionekana kuvurugika kutokana na mgawanyiko uliojitokeza kwenye Bunge
la Katiba, lakini katika uhalisia wake, hauna matatizo mengi

Post a Comment