MKE WA MTU ANASWA AKIZINI KWENYE GARI


BIASHARA ya kuuza miili imezidi kushamiri katika viunga vya Jiji la Mwanza na mwanzoni mwa wiki hii Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kilifanya zoezi lingine kubwa baada ya kumnasa mwanamke mmoja akifanya mapenzi ndani ya gari katika eneo la Kirumba, Ijumaa lina data kamili.
Mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu.
Baada ya kutajiwa maeneo yanayosifika kwa biashara hiyo maarufu kama uchangudoa, OFM ambao juzikati walilifumua danguro lililopo maeneo ya Liberty jijini hapa, Jumanne wiki hii lilifanya matembezi katika eneo hilo ili kubaini jinsi biashara hiyo haramu inavyofanyika.
Majira ya saa tisa za usiku, katika eneo lililopo jirani na Villa Park, OFM ilishuhudia wanawake wengi wakiwa wamesimama na kujinadi kwa wanaume waliokuwa wakiwafuata na kuzungumza nao biashara kama wauzao vitu halali.
Baadhi ya waliokubaliana waliondoka kuelekea kusikojulikana na wengine, walisogea pembeni na ‘kujisevia’ kwenye maeneo ya giza.Lakini katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja akiwa na mwanaume, alionekana akiingia katika gari moja lililokuwa limeegeshwa katika eneo linalojulikana kama Magereji, lililopo pembeni ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa na OFM lilipowafuatilia, liliwabamba wakifanya mapenzi.
Akishuka kwenye gari.
Wakati wakianza kupigwa picha mfululizo, mwanaume alifanikiwa kukimbia kwa kupitia dirishani na kutokomea bila kunaswa na kamera, wakati mwanamke alijikuta katika fedheha kubwa na kuanza kuomba msamaha kuwa picha yake isisambazwe kwa vile ataaibika.
Ijumaa: Sasa kwa nini unafanya biashara hii?
Mke wa mtu: Ni shida tu jamani, mume wangu kanitelekeza, naombeni mnisaidie msinitoe gazetini maana ndugu zangu wala hawajui kama nafanya biashara hii?
Baadaye katika uchunguzi wake, OFM ilibaini kuwa mlinzi wa gereji iliyopo eneo hilo ndiye amekuwa akitoa nafasi ya makahaba hao kutumia magari yanayolazwa eneo hilo kwa kuwatoza kiwango cha fedha ambacho hata hivyo hakikufahamika mara moja ni kiasi gani.
Hata hivyo, uchunguzi wa OFM umebaini kuwa machangudoa wengi wanaojiuza katika vijiwe vya Mwanza, wanatoza kati ya shilingi elfu nane hadi kumi kwa huduma ya muda mfupi, wakati wale wanaohitaji kulala nao, wanalipishwa kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000.
Ijumaa linalaani biashara hii na linawatahadharisha wanaoifanya kuiacha la sivyo yatawakuta makubwa ikiwa ni pamoja na kuaibika kwa picha zao kuanikwa gazetini.

Post a Comment

Previous Post Next Post