BIASHARA ya kuuza miili imezidi kushamiri katika viunga vya Jiji la Mwanza na mwanzoni mwa wiki hii Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kilifanya zoezi lingine kubwa baada ya kumnasa mwanamke mmoja akifanya mapenzi ndani ya gari katika eneo la Kirumba, Ijumaa lina data kamili.
Mwanamke huyo anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu.
Baada ya kutajiwa maeneo yanayosifika kwa biashara hiyo maarufu kama
uchangudoa, OFM ambao juzikati walilifumua danguro lililopo maeneo ya
Liberty jijini hapa, Jumanne wiki hii lilifanya matembezi katika eneo
hilo ili kubaini jinsi biashara hiyo haramu inavyofanyika.
Majira ya saa tisa za usiku, katika eneo lililopo jirani na Villa
Park, OFM ilishuhudia wanawake wengi wakiwa wamesimama na kujinadi kwa
wanaume waliokuwa wakiwafuata na kuzungumza nao biashara kama wauzao
vitu halali.
Baadhi ya waliokubaliana waliondoka kuelekea kusikojulikana na
wengine, walisogea pembeni na ‘kujisevia’ kwenye maeneo ya giza.Lakini
katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja akiwa na mwanaume, alionekana
akiingia katika gari moja lililokuwa limeegeshwa katika eneo
linalojulikana kama Magereji, lililopo pembeni ya Uwanja wa CCM Kirumba
jijini hapa na OFM lilipowafuatilia, liliwabamba wakifanya mapenzi.
Akishuka kwenye gari.
Wakati wakianza kupigwa picha mfululizo, mwanaume alifanikiwa
kukimbia kwa kupitia dirishani na kutokomea bila kunaswa na kamera,
wakati mwanamke alijikuta katika fedheha kubwa na kuanza kuomba msamaha
kuwa picha yake isisambazwe kwa vile ataaibika.
Ijumaa: Sasa kwa nini unafanya biashara hii?
Mke wa mtu: Ni shida tu jamani, mume wangu kanitelekeza, naombeni mnisaidie msinitoe gazetini maana ndugu zangu wala hawajui kama nafanya biashara hii?
Mke wa mtu: Ni shida tu jamani, mume wangu kanitelekeza, naombeni mnisaidie msinitoe gazetini maana ndugu zangu wala hawajui kama nafanya biashara hii?
Baadaye katika uchunguzi wake, OFM ilibaini kuwa mlinzi wa gereji
iliyopo eneo hilo ndiye amekuwa akitoa nafasi ya makahaba hao kutumia
magari yanayolazwa eneo hilo kwa kuwatoza kiwango cha fedha ambacho hata
hivyo hakikufahamika mara moja ni kiasi gani.
Hata hivyo, uchunguzi wa OFM umebaini kuwa machangudoa wengi
wanaojiuza katika vijiwe vya Mwanza, wanatoza kati ya shilingi elfu nane
hadi kumi kwa huduma ya muda mfupi, wakati wale wanaohitaji kulala nao,
wanalipishwa kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000.
Ijumaa linalaani biashara hii na linawatahadharisha wanaoifanya
kuiacha la sivyo yatawakuta makubwa ikiwa ni pamoja na kuaibika kwa
picha zao kuanikwa gazetini.
Post a Comment