EXCLUSIVE!
Kile kisa cha mtalaka wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhani
Nkongo ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ kuteswa na kudhalilishwa
nchini Afrika Kusini kisa kikidaiwa ni kudhulumu mzigo wa
wafanyabiashara wenzake kimeingia awamu nyingine!
Majeraha ya mgongoni aliyopata, Jumanne Hassan ‘Tevez’ wakati wa kuteswa.
KWANZA SIKU YA TUKIO
AMANI LAMSAKA
MSIKIE SASA
‘Tevez’ akiwa salama nyumbani kwake.
UKWELI NI UPI?
ULICHOPOTEZA KATIKA UTESWAJI
HAIKUWA KAZI RAHISI
KINACHOKUUMA NINI?
‘Tevez’akiwa na mwanaye.
KUHUSU KUKATWA NYETI, KUFANYIWA KITU MBAYA
SABA WAMEKAMATWA
BONGO LINI TEVEZ?
HALI YAKO KWA SASA
“Kusema
ukweli naendelea vizuri ni majeraha tu ambayo hata hivyo yanakauka. Ila
hili la pasi mgongoni ndiyo linasumbua kwa mbali, lakini naamini
litakaa sawasawa.
Kwa
mara ya kwanza Gazeti la Amani limeweza kuzungumza na Tevez kwa dakika
arobaini na tano kutokea nchini humo ambako anauguza majeraha.
Majeraha ya mgongoni aliyopata, Jumanne Hassan ‘Tevez’ wakati wa kuteswa.
KWANZA SIKU YA TUKIO
Kabla
Tevez hajasimulia kilichompata na hali yake kwa sasa, ni muhimu
kukumbuka kuwa, tukio hilo ambalo lilikuwa habari ya Jiji la Dar es
Salaam, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo picha zake zilizagaa
zikimuonesha akiwa amefungwa kamba huku mwili wake ukiwa umetapakaa
damu na majeraha kadhaa.
AMANI LAMSAKA
Kwa
vile habari za tukio hilo ziliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari
bila kupata balansi (uwiano) na Tevez mwenyewe, Amani liliingia kazini
kumsaka mhanga huyo usiku na mchana.
MSIKIE SASA
Akizungumza kwa hisia kali na gazeti hili juzi, Februari 3, mwaka huu kutoka Mji wa Durban, Afrika Kusini, Tevez alisema:
“Kusema
ukweli tukio lililonikuta watu huko nyumbani (Bongo) wanalitafsiri
tofauti sana. Nimesikia kwamba wanasema eti nilidhulumu mzigo wa mtu,
ndiyo maana niliteswa! Si kweli.”
‘Tevez’ akiwa salama nyumbani kwake.
UKWELI NI UPI?
“Ishu iko hivi, mwenyeji wangu hapa Durban, anaitwa Ibra, ndiye ambaye alinipokea siku nilipotua hapa.
“Huyu bwana inaonekana ni tamaa. Aliniundia njama, aliita wenzake na kuniteka kisha kunitesa sana wakidhani nina pesa nyingi.
“Niliteswa sana kwa kweli. Kama mlivyoona picha. Nilidhalilishwa sana, lakini katika yote ukweli sijadhulumu mzigo wa mtu.”
ULICHOPOTEZA KATIKA UTESWAJI
“Katika
mateso yangu, walifanikiwa kunipora Dola za Marekani elfu 14 (kama
shilingi milioni 22) na Landi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000)
zikiwemo simu zangu mbili aina ya Sumsung na Nokia ambayo nilikuwa
naitumia sana kuwasiliana na watu wangu muhimu.”
HAIKUWA KAZI RAHISI
Tevez
akazungumzia jinsi jamaa walivyomkamata: “Jamaa siku wananiteka usiku
kiukweli nilipambana nao sana hadi wanafikia hatua ya kunizidi nguvu na
kunifunga kamba. Nilikuwa nimewachapa kwelikweli ila kwa vile walikuwa
wengi na walikuwa wakitumia silaha nilijikuta nikiishiwa nguvu baada ya
kunipiga na kitu kizito kichwani nikapoteza fahamu, nilipojitambua ndiyo
nikakuta wamenifunga kamba.”
KINACHOKUUMA NINI?
“Tukio
linaloniuma zaidi ni yule jamaa ambaye anaonekana katika picha amekaa
jirani na mimi, hana shati. Alinichoma pasi mgongoni, namchukia sana
lakini nimemwachia Mungu.”
‘Tevez’akiwa na mwanaye.
KUHUSU KUKATWA NYETI, KUFANYIWA KITU MBAYA
Tevez:
“Nasikia watu huko Tanzania wanazusha eti nimekatwa nyeti, si kweli
kabisa. Mimi nimepigwa na kuchomwa pasi wala hakuna kitu kama hicho
zaidi ya kunichoma na pasi.
“Nimesikia
wengine wanasema nimetobolewa macho, huo ni uzushi wa watu tu! Mimi
niko safi na hali yangu ya kiafya inaendelea vizuri.”
SABA WAMEKAMATWA
Tevez
tena: “Nashukuru sana serikali ya huku wameweza kunisaidia kwani mpaka
sasa ninapoongea na wewe Musa Mateja hawa jamaa wamekamatwa saba.
“Jana
(Jumatatu) walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya
kunishambulia na kupora fedha. Wanatarajiwa kurejea tena mahakamani
baada ya siku 7, ingawa nimeambiwa kesho (jana Jumatano) wataletwa
Polisi Central ya huku kwa ajili ya mimi kuwatambua zaidi.”
BONGO LINI TEVEZ?
“Bongo
natarajia kurudi Alhamisi (leo) au Ijumaa (kesho) kama mambo yangu
yatakuwa kwenye mstari ila pia sasa hivi natarajia kuwasiliana na balozi
wetu ili nijue kama ana taarifa zangu na namna ambavyo ataweza
kunisaidia kama kiongozi wangu.”
HALI YAKO KWA SASA
Post a Comment