MWENYEKITI WA JKT NILILAZIMISHWA NIFANYE MAPENZI

HALI bado ni tete kwa mwenyekiti wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini wakakosa ajira, George Mgoba kufuatia kutekwa kwake na kujeruhiwa vibaya hivi karibuni na watu ambao bado hawajajulikana.
Mwenyekiti wa vijana waliofuzu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lakini wakakosa ajira, George Mgoba akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
Mgoba ambaye mpaka juzi alikuwa bado amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana jiijini Dar es Salaam baada ya kujeruhiwa, simulizi yake inaonesha kichwani kumejaa msongo mkubwa wa mawazo kutokana na watu waliomteka kumlazimisha kufanya mapenzi na mwanamke mmoja.
Kwa mujibu wa Mgoba, mwanamke huyo alikuwa mweupe, ana umri wa kati na wakati wanamlazimisha kufanya naye mapenzi yeye hakuonesha kukerwa, inaonekana alikuwa anajua.
“Kilichonishinda kufanya naye mapenzi yule mwanamke ni mwili kuishiwa nguvu na pia sehemu zangu za siri zilikuwa zina maumivu makali sana. sijajua nia yao ilikuwa nini kama ningefanikiwa,” alisema Mgoba.
Habari kutoka chanzo kimoja ndani ya jeshi la polisi, mwanamke huyo alitakiwaa kutumika maalum ili Mgoba aseme kila kitu kwa maswali ambayo angeulizwa na waliomteka.
“Ile ni njia ya kupata ukweli, huwa inatumika. Mtu anaweza kupewa mwanamke afanye naye mapenzi kwa lengo la kumchunguza. Si unajua wanaume wanapobanwa kwenye kona ya mahaba wanajiachia hata kwa mambo ya siri wao wanasema tu,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “We unadhani Samson (kwenye Biblia), kama si yule mwanamke wake Delila angesema siri ya nguzu zake?”Baadhi ya watu wameunganisha kitendo cha kutekwa kwa Mgoba kilichotokea Ijumaa iliyopita, Mabibo Dar na kwenda kutupwa mkoani Pwani ni harakati zake za kuwaongoza wenzake kuandamana kwenda Ikulu, Dar kwa lengo la kuonana na Rais Kikwete kudai wapewe ajira.
Juzi saa mbili na nusu asubuhi, Uwazi lilifika Hospitali ya Amana baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba, Mgoba ataongea na waandishi wa habari. Hata hivyo, mpaka Uwazi linaondoka saa tisa, Mgoba hakufanya hivyo huku polisi wanaomlinda na wauguzi wanaomtibu wakidai hawana mamlaka ya kumruhusu majeruhi huyo kuzungumza na vyombo vya habari.

Post a Comment

Previous Post Next Post