Dar esSalaam. Rais Jakaya Kikwete amesema Tanzania imeanza kukimbia kwa kasi kuelekea kwenye mafanikio makubwa yanayotarajiwa katika muda wa miaka 10 ijayo hivyo lazima wataalamu wazawa wapatikane ili kulinda rasilimali za taifa.
Akizungumza leo kwenye uzinduzi wa Sera ya elimu
Rais Kikwete amesema Serikali imeanza kujidhatiti mapema kwa kuanza
maandalizi huku elimu ikiwa kipaumbele cha kwanza katika kufikia malengo
hayo kwani bila elimu Tanzania haiwezi kujiendesha wenyewe.
Amebainisha kuwa ukuaji wa uchumi kwa asilimia
saba kwa mwaka unahitaji wataalamu wazawa watakaosimamia sekta
mbalimbali za uzalishaji, na kuongeza kuwa Ushirikiano wa kimataifa pia
unataka watu wenye uelewa wa mambo mengi ya ulimwengu pamoja na upanuzi
wa ajira.
“Maisha bora yanaletwa na elimu inayomsaidia mtu
kukabiliana na mazingira yanayomzunguka. Ni lazima tubadilike kulingana
na mahitaji yaliyopo. Serikali sasa hivi inafikiria kumgawia kila mtoto
kompyuta mpakato. Mambo mengi ya zamani ni lazima tuachane nayo,”
amesema Rais Kikwete.
Rais Kikwete amebainisha kuwa mabadiliko ya Sera
ya Elimu yamefanywa katika wakati muafaka ikiwa ni baada ya kuyavuka
malengo mawili ya millennia. Lengo la milenia kuhusu elimu ya msingi
pamoja na usawa wa kijinsia.
Ameeleza kuwa kama hayo yote tumefanikiwa
kuyafikia basi hata lengo la kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025
itawezekana na kwamba elimu ni lazima iwaandae watu kufika huko.
“Kilichodumaza elimu yetu ni kujilinganisha na
majirani zetu ambao tunawazidi kwa eneo na idadi ya watu pia. Lakini
baada ya kulibaini hilo na kuchukua hatua mabadiliko yanaanza kuonekana.
Tunataka tuwe na elimu bora katika nchi za Afrika Mashariki,” alisema.
Ametoa takwimu kuwa zinathibitisha kuwa baada ya
muda mfupi tutaizidi Kenya ambayo ndiyo iliyo juu kwa sasa katika
udahili wa wanafunzi katika ngazi zote kuanzia msingi mpaka chuo kikuu.
Amesema kuwa mwaka 2005 kenya ilikuwa na wanafunzi
925,340 katika shule za sekondari pamoja na 108,470 vyuo vikuu
ikifuatiwa na Uganda wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi wasiofika hata
nusu yake. Ilikuwa na wanafunzi 40,719 vyuo vikuu.
Post a Comment