Upelelezi
wa kesi ya kutotii amri halali ya polisi na kufanya mkusanyiko usio
halali inayowakabili wafuasi 30 wa Chama cha Wananchi (CUF)
haujakamilika.
Wengine
ni Allan Ally, Kaisi Kaisi , Abdina Abdina, Allawi Msenga, Mohamed
Mtutuma, Salehe Ally, Abdi Hatibu, Bakari Malija, Abdallah Ally , Said
Mohamed, Salimu Mwafisi, Saleh Rashid, Abdallah Said, Rehema Kawambwa,
Salma Ndewa, Athumani Said, Dickson Leason na Nurdin Msati.
Wakili
wa Serikali Joseph Maugo alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Emilius Mchauru wakati kesi hiyo
ilipotajwa.
Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 26, mwaka huu itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika.
Washitakiwa wanadaiwa Januari 27, mwaka huu , wilaya ya Temeke, washitakiwa wote walikula njama ya kufanya kitendo cha uhalifu.
Katika
mashitaka yanayowakabili mshitakiwa wa kwanza hadi wa 28, wanadaiwa
siku hiyo katika ofisi za CUF, karibu na Hospitali ya Temeke, bila
halali walifanya mkusanyiko kwa nia ya kufanya maandamano yasiyo halali
kwenda viwanja vya Mbagala Zakhem.
Aidha,
washitakiwa wanadaiwa siku hiyo katika eneo la Mtoni Mtongani, Temeke,
waligoma bila kujali tangazo halali lililotolewa na Polisi la kuzuia
kukusanyika na kuandamana isivyo halali.
Kwa
mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao ni Shabani Ngurangwa,
Shabani Tano au Kasakwa, Shabani Polomo, Juma Mattar, Mohammed Kirungi ,
Athumani Ngumwai, Shaweji Mohamed, Abdul Juma ,Hassan Saidi , Hemed
Joho , Mohamed Mbarouk na Issa Hassani.
Post a Comment