WATU wawili Maria Pajela [18] na William s/o Paschal [38] ,wote wakazi wa kijiji cha
Idweli, kata ya Isongole, tarafa ya Ukukwe wilayani Rungwe mkoani mbeya, wamekufa
baada ya kuungua moto kijijini hapo jana.
Taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya habari
leo, imesema kuwa, katika tukio hilo marehemu hao pamoja na baadhi ya wananchi wengine wa kijiji hicho walikuwa
katika harakati za kuiba mafuta kutoka katika gari t.891 aqz /t.821 arf aina ya
scania mali ya Ailis
Sanga lililokuwa limebeba mafuta aina
ya petroli ujazo wa lita 41,000, likitokea Dsm kuelekea nchini Malawi, likiendeshwa na dereva zawadi nyato [46] mkazi wa sae mbeya akiwa na tingo wake frank
yohana [24],mkazi wa mbozi.
Awali kabla ya tukio hilo gari hilo liliacha njia na
kupinduka, hivyo waathirika [dereva na tingo] walifanikiwa kuokolewa na
kupelekwa kituo cha polisi kiwira ili kupata hati ya matibabu [pf3] kwa ajili
ya kwenda hospitalini kupatiwa matibabu. hata hivyo baadhi ya wananchi wa eneo
hilo walivamia gari hilo na kufanikiwa kutoboa tanki la mafuta, hali
iliyopelekea mafuta kuanza kumwagika/kusambaa maeneo hayo na hata kuelekea
maeneo yenye makazi ya watu na wao
kukinga kwa kutumia vyombo vyao.
Katika tukio hilo watu kumi na nane [18] walijeruhiwa,
kati yao wanaume ni 13 na wanawake 05 ambao ni: 1. shukuru kanzale [21], 2.
nuru george [30], 3.asante boniface [38], 4. joseph jamson [18], 5.joseph
paschal [30], 6.siza kanesa [22], 7.alex
daud [35], 8. oscar yosia [23], 9.traiphon moasi [37], 10.samson mbwila
[29].
wengine ni 11. dora michael [35],12. veronica elia
[30],13.rabsen ayub [26], 14.wasiwasi spika [32], 15.asia anon [20], 16.bahati
kyando [23], 17. christopher erasto [32] na 18. melisa sanane [50], wote wakazi
wa kijiji cha idweli. aidha kati ya majeruhi hao,majeruhi 16 wamelazwa
hospitali ya misheni –igogwe na majeruhi wawili wamelazwa hospitali ya serikali
makandana-tukuyu na hali zao zinaendelea vizuri.
source:http://kalulunga.blogspot.com/

Post a Comment