Idara
ya usalama nchini Brazil imesema kuwa imewaua watu saba waliokuwa
wakifanya jaribio la kupora katika benk moja na ambao pia wanadaiwa
kujihusisha na dawa za kulevya.
Taarifa hizo zinasema kuwa
majambazi hao walianza kurushiana risasi na Polisi katika mji wa Novos
Kaskazin Mashariki mwa Brazil. Mtu mmoja anashikiliwa na Polisi,ambapo
pia bunduki na vifaa vya milipuko vilivyokuwa vinamilikiwa na watu hao
vinashikiliwa. Katika tukio jingine pia Polisi wamewaua watu wengine
wanne wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya katika mji
wa Rio de Janeiro. Kuuawa kwa majambazi hao kunafuatia mapambano ya
polisi na kundi hilo,ambapo mabomu na Bunduki vilikamatwa pia.
Post a Comment