Kocha
wa Barcelona Luis Enrique amemvulia kofia mshambuliaji wake Luis Suarez
na kusema nyota huyo analeta mambo matamu wiki hadi wiki.
Hiyo
ni baada ya mkali huyo wa Uruguay kutupia wavuni mabao mawili katika
ushindi wa bao 6-1 dhidi Rayo Vallecano kwenye mchezo wa La Liga.
Suarez alifungua kitabu cha magoli dakika ya 6 na akafunga kitabu hicho cha magoli dakika ya 90.
Lionel Messi akafunga mara tatu dakika ya 56, 63 na 68 huku beki Gerard Pique akifunga dakika ya 49 wakati goli pekee la Rayo Vallecano likifungwa na Alberto Bueno.
Kwa
magoli yake hayo matatu, Messi sasa analingana na Cristiano Ronaldo kwa
kutupia wavuni mabao 30 msimu huu, lakini pia anaweka rekodi mpya ya hat-trick 24 akimwacha hatua moja Ronaldo.
Barcelona:
Bravo, Pique, Xavi, Pedro, Iniesta (Rafinha 66), Suarez, Messi,
Mascherano (Rakitic 66), Alba (Adriano 76), Alves, Mathieu
Rayo
Vallecano: Alvarez, Tito, Amaya, Ba, Insua, Trashorras, Lica (Aquino
71), Jozabed (Quini 66), Bueno, Kakuta, Baptistao (Manucho 83)
Post a Comment