Jana,
Wakati akihojiwa na Mwanadada Shadee kwenye Kipindi cha Clouds E cha
Clouds TV, Msanii 'Fundi wa Muziki' kutoka nyumba ya vipaji THT, Barnaba
Elias 'Barnaba', pamoja na mambo mengi aliyozungumzia, alitoa maelezo
kuhusu wasanii watano anaowakubali na sifa zao Kimuziki ambapo alimtaja
Msanii wa BongoFleva Diamond Platnumz kuwa sio 'Mwanamuziki' mwenye
kujua kuimba muziki kiufundi.
Akifafanua
kauli yake kwa mapana , Barnaba alieleza kwamba Diamond hajui kuimba
kufuatana na alama zote muhimu za muziki, bali hutumia mtindo flani wa
kuimba 'kiujanja', mtindo ambao kwa wanaojua kuimba muziki technically
huwa wanautumia pale wanapofeli kufuata kanuni za uimbaji wakati
wakiimba.
Hata hivyo, alimsifia kwa kuwa 'mjanja' na kuweza kufanya muziki wake kuvutia na kuleta ladha.
Post a Comment