Mwenyekiti wa chama Chadema Freeman Mbowe.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwenyekiti wa
chama hicho Freeman Mbowe wamezindua operesheni ya vijana wa chama hicho
inayojulikana kama ‘Shahada mkononi delete CCM’.
Aidha, operesheni hiyo itasimamiwa na baraza la vijana wa chadema (
Bavicha ), katika mkutano huo Mbowe amewataka watanzania kuacha
kujengeana chuki za kisiasa na kuwa na upendo kama taifa moja kwani
vyama vya siasa ni mambo ya mpito.
Akizungumzia lengo la operesheni hiyo iliyozinduliwa wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mahakama ya mwanzo
nguzo nane mjini Shinyanga Freeman Mbowe amesema ni kuwahamasisha
vijana wenye umri wa kupiga kura kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi
mkuu wa oktoba mwaka huu.
Amewasisitiza wananchi juu ya kuchagua viongozi bora watakaowaondoa
kwenye lindi la umaskini uliokithiri, kuleta haki na usawa kwa watu
wote bila ubaguzi pamoja na kujenga jamii iliyo huru kiuchumi kwa
kutumia fursa mbalimbali zitokanazo na raslimali za taifa.
Baada ya uzinduzi wa operesheni hiyo mwenyekiti wa Bavicha taifa
Patrobas Katambi aligawa baiskeli 17 zilizotolewa kwa uongozi wa kata
zote za jimbo la Shinyanga mjini ambazo zitarahisisha zoezi la
uhamasishaji wa wananchi kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha

Post a Comment