TAHADHARI ichukuliwe! Habari zikufikie kuwa, baada ya
staa mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz‘ na mpenzi
wake, Zarinah Hassani ‘Zari’, kuhamia kwenye mjengo wake mpya uliopo
Madale jijini Dar, imebainika kuwa familia hiyo inaishi roho mkononi
kufuatia ulinzi sifuri, jambo linalowafanya kuishi kwa hofu tupu, Ijumaa Wikienda linakuhabarisha.
Nyumba mpya ya Diamond aliyohamia hivi karibuni.
TUJIUNGE NA CHANZO CHA HABARI
Kikizungumza kwa hofu juu ya familia hiyo, chanzo chetu makini
kilipasha kwamba, pamoja na Diamond kutumia mamilioni ya fedha kujenga
nyumba hiyo ya gharama kubwa, sasa changamoto imehamia kwenye ulinzi na
usalama wao.
Muonekano wa eneo ilipo nyuma ya Diamond iliyopo Madale jijini Dar.
“Jamani watu wanampongeza Diamond kwa kuhamia nyumba mpya lakini wale jamaa aisee wanapaswa kuombewa kila kukicha.
“Pamoja na kushusha mjengo wa maana bado changamoto ni juu ya ulinzi wao.
DIAMOND ANAISHI KIZAMANI?
Nasbu Abdul "Diamond" akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassani "Zari".
“Huwezi kuamini Diamond bado anaishi kizamani sana na sijui kwa nini
anajiamini kiasi hicho wakati anajua wazi kuwa yeye ni staa wa Afrika na
hapaswi kuishi kwa ulinzi hafifu.
MAENEO HATARISHI?
“Nasema hivi kwa sababu hata maeneo anayoishi ni hatari sana kwake
hivyo anatakiwa kuwa na ulinzi mkali ili tu siku moja asije akafanyiwa
kitu ambacho taifa likaingia kwenye hasara ya kumpoteza nyota mkubwa
kama yeye.
“Nina uhakika asilimia mia moja Diamond hadi leo hajaanza hata kufanya process (taratibu) za kuchukua silaha (bastola).
“Mimi naijua vizuri Madale ni sehemu ambayo watu huwa wanavamiwa mara kwa mara na wanaishi kwa hofu kama Diamond anavyoishi.
HIKI NDICHO KINACHOMPONZA
“Kitu kingine kinachomponza Diamond ni ishu ya kuweka kila kitu
kilichopo ndani kwake mitandaoni. Usione kila mtu anasifia lakini kuna
wengine wanavitolea macho.
“Kwa mfano katupia picha za toilet (choo) ambacho kimepakwa dhahabu na kusema kimegharimu shilingi milioni 70.
“Hajakaa sawa akatupia picha za jikoni kwake kuna vitu vingi vya
thamani kubwa kila mahali mpaka kwenye korido kuna flat screen
(runinga). Huko si ni kuwakejeli watoto wa mbwa? Ni vizuri akaacha
kufanya hivyo kwa sababu anawapa watu tamaa,” kilitiririka chanzo hicho.
ANA ULINZI GANI?
Juu ya ulinzi wa nyumbani kwa Diamond, chanzo hicho kilidai kwamba,
mbali na baunsa anayewalinda aitwaye Mwarabu hakuna askari wa silaha
anayelinda nyumbani hapo hivyo jamaa anatakiwa kufanya haraka kuajiri
walinzi wenye silaha.
BOFYA HAPA KUMSOMA DIAMOND
Baada ya habari hizo na uchunguzi wa kutosha, Ijumaa Wikienda lilimsaka Diamond a.k.a Dangote au Chibu ili kujua namna anavyoishi na jinsi anavyoimarisha ulinzi wake na familia kwa jumla.
Diamond, mbali na kukiri kuwa na hofu, alikuwa na haya ya kusema:
“Suala la ulinzi wangu nalijua mwenyewe lakini zaidi watu wanatakiwa
kujua mimi nipo na mlinzi na ninaendelea kuimarisha ulinzi wa nyumbani
kwangu.
“Sidhani pia kama ni suala zuri sana kwa watu kujua siri za ulinzi
wangu ila mambo mengi ya kujilinda niko kwenye michakato ya mwisho
kukamilisha na soon (haraka) mambo yote yatakaa levo maana huwezi
ukafanya kila jambo kwa wakati mmoja,” alisema Diamond huku akikubaliana
na ushauri wa gazeti hili juu ya kuongeza ulinzi alionao wa baunsa.
ILIWAHI KUMTOKEA SUGU
Huko nyuma iliwahi kumtokea Mwanamuziki Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye
kwa sasa ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) ambapo alikuwa amerejea
kutoka nchini Uingereza.
Akiwa amepanga nyumba nzima maeneo ya Tegeta, Dar, Sugu alifanyiwa
makala ya runingani na kuonesha vitu vya thamani vya nyumbani kwake.
Siku chache baada ya kipindi hicho kuruka runingani, jamaa huyo alivamiwa na kuporwa kila kitu lakini yeye hakudhurika
Post a Comment