Kha! Hata kabla ya siku 40 baada ya kifo cha baba yake, Ebby Sykes
aliyefariki wiki mbili zilizopita, legendary wa Bongo Fleva, Abdul Sykes
‘Dully Sykes’ amenaswa klabu ya usiku akiwa na totoz za kumwaga hivyo
kuibua minong’ono na mshangao ikidaiwa kwamba ni mapema mno kujirusha.
...Akijiachia na moja ya totoz hizo.
“Jamani yule si Dully ambaye amefiwa na baba yake juzi tu? Mbona
amegandana na yule mrembo kule ukutani? Hebu waangalie wanafanya nini
jamani? Duh! Kweli haya ni mambo ya kizungu,” alisikika mdada mmoja
aliyeonekana kuwapiga chabo kwenye giza huku akimsisitiza mwenzake naye
apige chabo.
Kufuatia tukio hilo, mwanahabari wetu alimfuata Dully kisha akampa
pole na kumuuliza kulikoni kujivinjari klabu usiku huo uliokuwa
ukielekea mishale ya saa nane na ushee?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Dully alipokea pole kisha akamwaga utetezi wake:
“Nimetokea
kwenye kikao cha kupanga hitima ya marehemu baba, nimeona nipitie hapa
kupoza machungu ya msiba na kumsalimia swahiba wangu, Banana Zorro.”
Wadau waliokuwa ukumbini hapo walisema ni kawaida kwa mtu mwenye
mawazo kujivinjari sehemu kama hiyo kupunguza mawazo na haina maana
kujifungia ndani na kulia.
legendary wa Bongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ akiwa na totoz.
Staa huyo wa Ngoma ya Togola alinaswa na Ijumaa Wikienda ndani ya
Club East 24 iliyopo Mikocheni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo
jamaa alikuwa bize akifanya yake bila kujali mashabiki waliokuwa
wakimshangaa wakati B-Band chini ya Banana Zorro ikifanya makamuzi.
Wakati makamuzi ya bendi hiyo yakiwa yamepamba moto, Dully alionekana akikumbatiwa kimahaba na mrembo mmoja baada ya mwingine.
...Akijiachia na moja ya totoz hizo.Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Dully alipokea pole kisha akamwaga utetezi wake:

“Nimetokea
kwenye kikao cha kupanga hitima ya marehemu baba, nimeona nipitie hapa
kupoza machungu ya msiba na kumsalimia swahiba wangu, Banana Zorro.”
Wadau waliokuwa ukumbini hapo walisema ni kawaida kwa mtu mwenye
mawazo kujivinjari sehemu kama hiyo kupunguza mawazo na haina maana
kujifungia ndani na kulia.
Post a Comment