Rais wa Liberia, Ellen Johson Sirleaf
Rais
wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametoa wito wa kuwepo mipango ya
kusaidia nchi za Magharibi mwa Afrika zilizoathiriwa kwa Ugonjwa wa
Ebola.
Wito wake umekuja baada ya Sierra Leone kupatiwa kiasi cha
Dola milioni 80 za Marekani ili kumaliza tatizo la Ebola na madhara
yaliyotokana na Ugonjwa huo.
Shirika la fedha duniani, IMFlimeahidi kutoa msaada wa kiasi cha dola milioni 187 kwa Sierra Leone.
Takriban dola bilioni 5 zimeahidiwa kimataifa kupambana na maradhi ya Ebola.
Ujumbe
wa takriban watu 600 duniani umekutana mjini Brussels siku ya jumanne
kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Ebola na mipango ya muda mrefu kupambana
na Ugonjwa huo.
Takriban Watu 10,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, wengi wao nchini Guinea,Liberia na Sierra Leone

Post a Comment