Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu
wawili wanaojiita ni viongozi wa watu waliopitia mafunzo ya mgambo kwa kosa la
kuratibu na kuongoza vikao vya uchochezi vya mgambo dhidi ya serikali.
Watuhumiwa hawa wanajulikama kwa majina ya MATHIAS S/O LUBEGA, Miaka
43, Mkazi wa Bunju, aliyekamatiwa Mission Pub maeneo ya Mbagala Mkoa wa
kipolisi Temeke. Wa pili anaitwa MG 437236 MOHAMED S/O ALLY, Miaka 28, Mkazi wa
Mbagala Zakhiem ambaye alikamatiwa maeneo ya Temeke alikokuwa amejificha.
Watu hawa wamekuwa wakikutana mara kwa mara jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kupata idadi kubwa ya wanamgambo ambao watawaunga mkono katika malengo
yao. Pia wamekamatwa na nyaraka mbalimbali za uchochezi zenye lengo la
kuwashawishi wanamgambo kuamka na kutambua kuwa wananyimwa haki zao na
serikali.
Taarifa za awali zinaonyesha kwamba lengo lao kuu ni kuwakusanya
kuwapotosha wenzao ili kuleta uvunjivu wa amani kupitia madai ambayo hayana
msingi wowote wa kisheria.
Natoa wito kwa wanamgambo wote waendelee kuwa waadilifu na kuzingatia
mafunzo yao ya uzalendo na ukakamavu na kuwa tayari kuitumikia nchi yao
kutokana na maelekezo na sio kwenda kinyume na hapo.
MAJAMBAZI SUGU SABA WAKAMATWA NA SILAHA JIJINI DAR ES SALAAM
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendesha
oparesheni kamambe katika maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam ambapo limepata
mafanikio kam ifuatavyo:
1. KUKAMATWA KWA SILAHA NA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI
Kuanzia tarehe 05/03/2015 hadi sasa zimekamatwa silaha tatu aina
tofauti na watuhumiwa saba wakihusishwa na silaha hizo wakizitumia katika matukio
mbalimbali ya ujambazi.
Tarehe 06/03/2015 huko Mwananyamala ilikamatwa Bastola aina ya REVOLVER
yenye namab 106108074 TZCAR96093 ikiwa na risasi 12 pamoja na watuhumiwa
watatu. watuhumiwa hawa walikamatwa baada ya kupatikana kwa taarifa toka kwa msiri.
Watuhumiwa hao ni:
a:
RAMADHANI S/O MASANJA MHAMBO, Miaka 34, Baharia, Mkazi wa Mwananyamala.
b: ELIAZR S/O JACKOB NKURARUMI @ JUMA ADAM
MOHAMED, MRUNDI, Miaka 25, Mlinzi wa
Colombia Hotel, Mkazi wa Tandale.
c: RAJAB S/O NASSORO, Miaka 30, Fundi Simu, Mkazi
wa Mwananyamala kwa Sindano.
Aidha tarehe 07/03/2015 maeneo ya Mbagala kizuiani walikamatwa
watuhumiwa wawili wakiwa na bunduki moja aina ya SHORTGUN PUMP ACTION yenye
namba R216145 TZCAR79067 ikiwa na risasi mbili. Watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo:
a: SAID S/O ZUBER
KIBWANA @ BAKHRESA, Miaka 33, Mkazi wa Mbagala.
b: OMAR S/O NZEGULA MPONDAMALI, MIAKA 29, Mkazi wa
Kigamboni Mikwambe.
Watuhumiwa wengine wawili walikamatwa wakienda kufanya tukio maeneo ya
Namanga Mkoa wa Kipolisi Kinondoni lakini waliwekewa mtego na polisi na
kukamatwa kabla hawajafanya tukio hilo. Walikamatwa wakiwa na Bastola aina ya
BROWNING COURT yenye nambari A558651 na risasi kumi. Watuhuniwa wananendelea
kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake.
KUKAMATWA KWA DOLLA ZA KIMAREKANI ZIPATAZO 426
ZINAZODHANIWA KUWA NI BANDIA.
Aidha, msako huu unaoendelea umefanikisha kukamatwa kwa noti bandia za
Dolla za Kimarekani zipatazo 426 ambapo noti 36 ni za Dolla 100 na noti 390 ni za Dolla 50.
Dola hizi bandia zimekamatwa kwa watuhumiwa RAMADHANI S/O MASANJA
MHAMBO, Miaka 34, Baharia, Mkazi wa Mwananyamala; ELIAZR S/O JACKOB NKURARUMI @
JUMA ADAM MOHAMED, MRUNDI, Miaka 25,
Mlinzi wa Colombia Hotel, Mkazi wa Tandale; na
RAJAB S/O NASSORO, Miaka 30, Fundi Simu, Mkazi wa Mwananyamala kwa
Sindano, walipopekuliwa kwenye makazi yao.
Noti hizo zikibadilishwa katika pesa za kitanzania ni sawa na shilingi
za kitanzania 42,504,000/= (Millioni
arobaini na mbili, mia tano na nne elfu)
Jeshi la Polisi linawatahadharisha watanzania kuwa makini wanapofanya manunuzi au biashara yoyote kwa sababu wanaweza kuangukia katika mtego wa kupewa noti bandia.
Post a Comment