Hatma ya ACT 25 Machi, 2015

CHAMA kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania) sasa kimetinga mahakamani.


Lucas Kadavi Limbu, mmoja wa waasisi na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, amefungua shauri Na. 17 la mwaka 2015 dhidi ya Samson Mwigamba ambaye ni katibu mkuu wa muda na Peter Mwambuja na Masange M. Masange.

Katika shauri hilo la madai, lililofunguliwa Mahakama Kuu, kanda ya Dar es Salaam, Limbu anataka mahakama itoe amri ya kumzuia Mwigamba na “mawakala wake,” kujihusisha na chama hicho; kukiongelea katika vyombo vya habari na kutoa maelekezo yoyote yale kwa wanachama na viongozi wake.

Wadai wengine katika shauri hilo, ni naibu katibu mkuu (Bara); Grason Nyakarungu, katibu mwenezi na mwenyekiti wa vijana taifa; na Ramadhani Suleiman, makamu mwenyekiti (Zanzibar).

Kesi hii imetajwa kwa mara ya kwanza leo na imepangwa kusikilizwa tarehe 25 Machi mwaka huu, ambako mahakama itasikiliza maombi ya kuzuia mkutano mkuu wa chama.

Kabla ya kujiunga na ACT-Tanzania, Mwigamba alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Arsha. Alifukuzwa uanachama mwaka mmoja uliopita.
- Chanzo JF

Post a Comment

Previous Post Next Post