Ikiwa
ni siku moja tu imepita tangu aliyekuwa mbunge wa jimbo la
kigomakaskazini ZITTO KABWE (CHADEMA) kungatuka rasmi na kuuacha
ubunge,kiongozi huyo anatarajiwa kutambulishwa rasmi na kupewa kadi ya
chama cha ACT TANZANIA kesho jumapili tarehe 22 mwezi wa tatu mwaka 2015
jambo ambalo linatarajia kuandika historia mpya
Kwa
mujibu wa taaarifa iliyotolewa na afisa habari wa ACT TANZANIA jioni
hii kwa mtandao huu inadai kuwa ZITTO KABWE atatambulishwa ndani ya
chama hicho kipya kesho mbele ya wanahabari katika hoteli ya serena
mnamo saa tano kamili asubuhi ambapo baada ya makabidhiano ya kadi ya
kukaribishwa rasmi atapata nafasi ya kuzngumza na wanahabari juu ta
chama chake hicho kipya.MTANDAO HUU UTAKUWA ENEO LA TUKIO KUKUPA KILA
KITAKACHOJIRI HAPO
Post a Comment