kikwete akamilisha ngwe ya uteuzi wa wabunge


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu  kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
-          Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
-          Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
-          Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
-          Mhe. Janet Zebedayo Mbene
-          Mhe. Saada Salum Mkuya
-          Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
-          Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
-          Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
26 Machi, 2015

Post a Comment

Previous Post Next Post