Mkali
wa long time kwenye muziki wa kizazi kipya Gwamaka Kaihula maarufu kama
Crazy GK amesema moja ya vitu vinavyowachanganya wasanii ni kupokea
kipato kikubwa kuliko walivyotarajia.
Akizungumza
na EFM Radio kupitia kipindi cha Genge wakati akitambulisha ngoma yake
mpya “Shukran”, GK akasema mara nyingi maisha ya wasanii yanabadilika na
wakati mwingine kuingia kwenye makundi mabaya kutokana na mafanikio
ambayo hawakuyatarajia na hali huwa mbaya zaidi pale mafanikio yake ya
ghalfa yanapotoweka.
“Sisi
wasanii wengi tunatokea kwanye maisha ya hali ya chini na pengine
tulikuwa hatutarajii makubwa sana. Unapiga hesabu za kupata laki moja
lakini badala yake unapata milioni tano, ni lazima uchanganyikiwe,”
alisema GK.
Mkali huyo wa kundi lililotamba sana East Coast Team (ECT) alisema inahitaji utulivu wa hali ya juu kwa msanii ili kulinda heshima yake na kuepuka kujiingiza kwenye makundi mabaya yakiwemo ya utumiaji madawa ya kulevya

Post a Comment