BAADA
ya kukulia katika maisha ya kimasikini kwa kipindi kirefu, Mwalimu Bora
wa Ujasiriamali nchini Tanzania, Eric James Shigongo anatarajia kuanza
semina ya ujasiriamali iitwayo KUTOKA UFUKARA MPAKA UBILIONEA, itakayofanyika Tandale jijini Dar es Salaam.
Lengo kubwa la kufanya semina hiyo ni kumkomboa kijana masikini
aishiye Tandale ahame kwenda sehemu ya watu wanajiona kuwa matajiri,
Masaki au Oysterbay na kwingineko, yote inawezekana.
Somo kubwa atakalofundisha ni Jinsi ya Kuhama Kutoka Kwenye Umasikini
Kwenda Kwenye Mafanikio. Katika semina hiyo, hatokuwa peke yake bali
kutakuwepo na walimu wengine maarufu Tanzania kama James Mwang’amba na
Dk. Didas Lunyungu, pia ili kuwaonyeshea vijana kwamba inawezekana,
msanii mwenye jina kubwa, aliyetokea uswahilini, Diamond Platnumz
atakuwepo kwa ajili ya kuzungumza na vijana.
Semina hiyo itaanza tarehe 2/4/2015 mpaka 4/4/2015 katika Uwanja wa
Gengeni (Kwa Sharifu) hapo Tandale Mbuyuni na hakutokuwa na kiingilio
chochote kama ilivyo sehemu nyingine, elimu yote hiyo itatolewa
BUREEEEE.
Karibuni sana.
Dk. Didas Lunyungu
Post a Comment