Msanii KEISHA apata ajali akitokea chuoni CBE

Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba, Posta jijini Dar.
Akizungumza na Clouds Fm alisema kuwa alikuwa akitoka chuoni CBE na kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo ndipo lilipotokea gari na kumuovateki na kuligonga gari lake. Aidha alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani.
“Nashukuru Mungu nilipimwa hospitali vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote kwa ndani kwani nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa ndani,” alisema Keisha.
Source: http://www.cloudsfm.co/

Post a Comment

Previous Post Next Post