MTI WA MLONGE NA MATATIZO YA MFUMO WA UZAZI KWA WANAWAKE-3

WIKI iliyopita tuliishia kwenye dalili za tatizo linaloitwa Pelvic Inflammatory Diseases (PID), leo tutajikumbusha dalili hiyo na tutaendelea na upande mwingine.
DALILI ZA PELVIC INFRAMATORY DISEASES (PID) Dalili ya kwanza ilikua ni hali ya kupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi ambayo kitaalamu inaitwa Dysmenorrheal, tulisema kwamba maumivu haya makali wakati wa hedhi yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni Primary Dysmenorrheal ambayo huwapata  wasichana ambao hawajapata watoto lakini pia kuna Secondary Dysmenorrheal ambayo huwapata wanawake ambao tayari wana watoto.
Maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa, hii humsababisha mwanamke kukosa raha hasa wakati wa tendo na kumsababishia akose hamu kabisa ya kushiriki tendo la ndoa lakini hii huweza kuwa inasababishwa sana na tatizo hili la PID na ikasababisha mwanamke huyu kukosa raha yeye mwenyewe na hata kusababisha migogoro katika ndoa yake na kumbe kama angelijua kwamba kuna mimea tiba ambayo husaidia sana kuondoa tatizo hili basi angeitumia, baadaye tutaelekezana jinsi ya kuondoa kabisa tatizo hili kwa kutumia mmea huu wa mlonge.
TATIZO LA FIGO Pia kuna hili suala la matatizo ya figo ambalo limekuwa ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi sana na hii ni kwa sababu wanawake wengi ni rahisi sana kukumbwa na tatizo la UTI yaani Urinary Truck Infections na hii ni kwa sababu mrija wao wa kupitishia mkojo (urethra) ni mfupi hivyo basi maambukizi ni rahisi sana kufika kwenye kibofu cha mkojo na kusambaa zaidi hasa kwenye mirija inayokwenda kwenye figo na pia tatizo kufika kwenye figo kwa urahisi zaidi.
Na hii ni kwa sababu wanapoenda haja huchutama na maumbile yao kuwa karibu sana na maeneo ya hatari na maambukizi ya UTI huweza kumpata mwanamke huyu, na sasa tatizo hili akishalipata na kutolitibu haraka au akawa anatibu lakini hailiishi kabisa maana kuna wakati mwanamke utakuta anasema tatizo linajirudia mara kwa mara kumbe tu halijaisha mwilini basi inakua ni rahisi sana kufika kwenye figo na kuanza kusumbuliwa na tatizo la figo.
Lakini mmea huu wa mlonge unaweza kukusaidia sana msomaji wetu pia tutawaelekeza jinsi ya kuutumia hapo nyumbani.
Na kwa wale ambao wamesumbuliwa sana na tatizo hili la UTI pia wamekuwa wakijitibia sana pasipo na mafanikio yoyote na wengine wameshachoma hadi sindano lakini tatizo hili bado linawasumbua basi ni vyema wawasiliane nasi kwani tuna mimea tiba mingi kwa ajili ya kutatua tatizo hili la UTI.
Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.

Itaendelea wiki ijayo

Post a Comment

Previous Post Next Post