Cristiano Ronaldo amefungia Real Madrid magoli mawili katika mchezo wa Ligi ya mabingwa dhidi ya Schalke 04 na kuipiku rekodi ya mpinzani wake mkubwa Lionel Messi.
Ronaldo anafikisha mabao 78 katika Ligi ya mabingwa (pamoja na UEFA Super Cup) huku Messi akiwa na magoli 76.
Lakini
nyota huyo wa Ureno analingana na Messi katika kufunga magoli mengi
kwenye Ligi ya Mabingwa (ukiondoa hatua ya mchujo) ambapo wote
wametikisa wavu mara 76.
Ronaldo
mwenye umri wa miaka 30 anaweka rekodi nyingine na kuwa mchezaji wa
kwanza wa Real Madrid kufunga magoli 40 na zaidi katika msimu mmoja kwa
misimu mitano mfululizo.
Messi
atakuwa na nafasi ya kumpiku Ronaldo Machi 18 wakati Barcelona
itakapoikaribisha Manchester City kwenye mchezo wao wa marudiaono wa
Ligi ya Mabingwa.

Post a Comment