NESI ANAYETOA SIRI ZA WAATHIRIKA WA UKIMWI MORO, ASUTWA KWA MATARUMBETA

KAMA kawa ni Ijumaa nyingine ambayo mapaparazi wetu, Musa Mateja ‘Toz’, Harun Sanchawa ‘Cheusi’, Dustan Shekidele ‘Mkude Simba Mzee wa Mji Kasoro Bahari’ na Mpigapicha Mkuu Richard Bukos walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kumjuza moja kwa moja mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge, jijini Dar.

Saa 2:13 usiku

Mkuu anaanza kumtwangia Mpigapicha Mkuu Richard Bukos aliyekuwa maeneo ya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar.

MADENTI FEKI WA UDSM WANASWA WAKIJIUZA CHUONI

Makao Makuu: Niambie Bukos, uko pande gani leo?

Bukos: Niko maeneo ya Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDSM) kwenye Pub f’lani iko huku upande wa Ardhi

Makao Makuu: Kuna nini?

Bukos: Nilisikia baadhi ya madenti wanajiuza maeneo haya na wanamalizia mambo yao hapa uwanjani hivyo nimejibanza sehemu napiga chabo.

Makao Makuu: Vipi umebaini kitu gani?

Bukos: Mkuu nimeshuhudia wababa wawili wakifanya mambo yao kwenye uwanja huo lakini wadada waliokuwa nao nahisi wanajifanya wanachuo lakini siyo kwa sababu baada ya kutoka kwenye shughuli yao nikawafuata na kuwahoji.

Makao Makuu: Wanasemaje?

Bukos: Mkuu nimebaini hawa machangu siyo wanachuo kwa sababu hata ‘vingereza’ vyao ni vya kiubabaishaji kuna mmoja nilipomsalimia kimombo How are you? Akanijibu ‘faini thank yuu tichaaa’ nikamuona kama mbabaishaji siyo msomi wa hapa.

Makao Makuu: Dah! Itabidi hilo eneo OFM mjipange ili mlifungie kazi.

 4:12 usiku

MAAFANDE WANASWA WAKISEREBUKA

Makao Makuu: Halooo halooo Sanchawa, uko wapi?

Sanchawa: Mkuu niko kituo cha Stakishari hapa Ukonga kuna burudani ya muziki maafande wanafanya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya na kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa kituo hiki, Idd Kyogomo yaani wanaserebuka mno.

Makao Makuu: Kwa hiyo leo kituoni ni furaha tu hata watuhumiwa hawawapokei.

Sanchawa: Aaah wapi hivyo tunavyoongea kuna njemba mmoja kaletwa msobemsobe na difenda alipofikishwa hapa akawa anadengua kushuka yaani sherehe ilisimama kwa muda kundi la maafande wakachomoka fasta kwenda ‘kumu-arest’ mpaka njemba akatoa kamasi na kuangua kilio huku akifuata maelekezo.Makao Makuu: Sawa Sanchawa piga kazi mimi ngoja nimsake, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’.

Saa 6:18 usiku

MKULIMA ALIZWA POCHI NA CHANGUDOA

Makao Makuu: Issa Mnally, naona umewasili toka Kanda ya Ziwa vipi upo pande zipi?

Mnally: Mkuu mimi nipo ndani ya Corner Bar hapa Sinza Afrika Sana lakini nimezama zaidi nipo kwenye ukumbi wa disko.

Makao Makuu: Ni kituko gani ulichokipata hapo.

Mnally: Kuna jamaa mmoja inaonekana ni mkulima kaja kuuza mazao yake sokoni Kariakoo, sasa alizuia mlangoni hamna mtu kutoka wala kuingia kisa amelizwa pochi na changudoa.

Makao Makuu: Huyo kajitakia basi aende akalime tena siku akija mjini aje kiadabu aachane na mambo ya machangu.

Saa 7:27 usiku

SHILOLE NUSURA AMPASUE MWIZI WA BIA YAKE

Makao Makuu: Halooo..halooo…Musa Mateja.

Mateja: Naam Mkuu wangu nakupata sawia bila mikwaruzo.

Makao Makuu: Uko wapi?

Mateja: Mkuu niko ndani ya Ukumbi wa Escape One kwenye Tamasha la Usiku wa Ishi Kistaa.

Makao Makuu: Duuh, kuna mastaa gani hapo?

Mateja: Mkuu ni wengi sana lakini karibu yangu nawaona Izzo Business, Barnaba, Linah, Stara Thomas, Rich Mavoko, Nuh Mziwanda, Shilole na wengine kibao.

Makao Makuu: Vipi kuna kituko chochote hapo?

Mateja: Mkuu kuna kijana anaitwa Customer Care, yeye kazi yake ni kupiga watu mizinga ya hela na pombe.

Makao Makuu: Kawafanyaje?

Mateja: Leo alichemka kila alipopiga mzinga watu wamemtolea nje sasa kajipenyeza kwenye meza ya kina Shilole na kumuibia pombe ndipo Shilole akamshtukia na kutaka kumpasua na chupa ya kichwa lakini wasamaria wema wamemtuliza mzuka.

Makao Makuu: Duh, Shilole naye hiyo sasa sifa kabia kamoja tu ndiyo ampasue mtu! Haya ngoja nimcheki Dustan Shekidele ‘Mkude Simba Mzee wa Mji Kasoro Bahari’.

Saa 8:02 usiku

NESI ANAYETOA SIRI...Makao Makuu: Halooo Shekidele habari za hapo Mji Kasoro Bahari?

Shekidele: Salama kabisa Mkuu wangu.

Makao Makuu: Haya niambie mida hii uko wapi na nini kinaendelea?

Shekidele: Mkuu nipo maeneo ya Mwembe Songo kuna nesi mmoja wa Hospitali kubwa ana tabia ya kuvujisha siri za waathirika wa Ukimwi na kuzitangaza mitaani sasa walikuwa wakimvizia na matarumbeta wakamsute ila inaonesha mwenyewe ameshtukia mchezo akawa hashindi nyumbani hivyo ndiyo hao wasutaji wameamua kumfungia kazi usiku huu wa manane ndiyo wamemkuta. Full kumsuta na kumzodoa.

Makao Makuu: Kha! Ndiyo akome huyo. Haya Mkude Simba wapigie wenzako uwaambie mkapumzike

Post a Comment

Previous Post Next Post