NGELEJA NAYE AFIKISHWA KIZIMBANI, AKIRI KUPOKEA MAMILIONI YA ESCROW


Mbunge William Ngeleja jana amepandishwa katika Baraza la Maadili ya viongozi wa umma kuhojiwa juu ya tuhuma zinazomkabili za kunufaika na mgawo zaidi ya Sh. milioni 40 kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Baraza hilo jana liliahirisha shughuli zake za kumhoji Mkurugenzi wa Sheria, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma  kutokana na shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni Komba katika viwanja vya Karimjee, eneo ambalo Baraza hilo linafanyia mahojiano hayo.
Wakati  Baraza likimhoji  Ngeleja leo, tayari limekwisha wahoji Wabunge Andrew Chenge na Prof. Anna Tibaijuka ambapo Baraza hilo litaendelea na shauri la Prof. Tibaijuka  Machi 13, mwaka huu baada ya Wakili wake Dk. Rugemaleza Nshala, kuomba udhuru wa kwenda Marekani kwa siku 10.
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji mstaafu Hamisi Msumi, alisema shauri hilo litaamuliwa kama liwe la uamuzi wa ndani au hadharani.
Kwa upande wa Chenge, tayari alikwishakata rufaa  katika Mahakama Kuu kuzuia shauri lake lisijadiliwe.

Post a Comment

Previous Post Next Post